• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
SONGWE REGION
SONGWE REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa MKOA WA SONGWE

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Sehemu
      • Mipango na Uratibu
      • Idara ya Elimu
      • Huduma za Maji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Huduma za Serikali za Mitaa
      • Miundombinu
    • Vitengo
      • Huduma za Kisheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
  • Wilaya
    • Mbozi DC
    • Songwe DC
    • Momba DC
    • Ileje DC
  • Halmashauri
    • Mbozi
    • Ileje
    • Momba
    • Songwe
    • Tunduma
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Mifugo
    • Madini
    • Kilimo
    • Biashara
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya na Ustawi Wa Jamii
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma ya Mifugo na Uvuvi
    • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
    • Mipango na Takwimu
    • Ujenzi
  • Machapisho
    • Sheria
    • Miongozo
    • Sera
    • Fomu za Maombi
    • Utaratibu
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

YALIYOJIRI KATIKA ZIARA YA KATIBU TAWALA MKOA WA SONGWE DAVID KAFULILA WILAYANI ILEJE

Posted on: February 13th, 2019

  Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila amefanya ziara Wilayani Ileje ambapo ameanza kwa kuzungumza na watumishi wa Halmashauri hiyo, amekagua Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Ileje na kutembelea kaya za Wanufaika wa Mpango wa TASAF ambapo haya ndiyo yaliyojiri;

  • Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila amekuja kuwakumbusha sheria, kanuni na taratibu za Utumishi wa Umma kwakuwa yeye ndiye Mkuu wa Utumishi wa Umma Mkoa wa Songwe- Katibu Tawala Msaidizi Utawala na Utumishi, Chele Ndaki
  • Napenda kuwakumbusha watumishi wote kuheshimu mamlaka zilizopo Kisheria na kuzingatia sheria zote za utumishi wa umma - Katibu Tawala Msaidizi Utawala na Utumishi, Chele Ndaki
  • Watumishi hakikisheni kuwa mnatimiza majukumu yenu wakati mnadai maslahi yenu yaani kama kuna mambo mnadai sio sababu ya kuweka uzembe katika utumishi wenu- Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila
  • Tulisaini Mkataba wa utumishi kwenye sekta za elimu na afya kwa kuwekeana vigezo ambavyo vitapimwa mwezi huu wa pili na mwezi wa tatu tutafanya tathmini, wale watakao shindwa kufikia vigezo hivyo tutawaondoa ili wawekwe wengine ambao watafanya vizuri - Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila
  • Kwa mujibu wa sheria za utumishi zinaruhusu mtumishi aliyeshindwa kutimiza wajibu wake kufukuzwa kazi au kunyang’anywa cheo, sio mpaka uibe - Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila
  • Kama taasisi wote tunatakiwa kuongeza ufanisi wa uendeshaji wa kazi zetu, kama Mkoa tumeanzisha mfumo wa kupima utendaji wa watumishi unaoitwa Songwe Task Information Management System, kwa mfumo huu tutakuwa wa kwanza kuutumia nchini na utawezesha kufahamu utendaji wa kila siku wa watumishi wote- Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila
  • Mtendaji yeyote atakaye shindwa kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli la kuhakikisha kila mjasiriamali mdogo anapatiwa kitambulisho, hususani kwa kipindi kilichobaki cha wiki tatu, hilo ni kosa ambalo linatosha kumfukuzisha kazi- Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila
  • Ujenzi katika Hospitali ya Wilaya ya Ileje Umesitishwa mpaka hapo kasoro zilizooneka zirekebishwe, awali ili ripotiwa kuwa kwenye beam kuna ufa na kusababisha mpasuko kwa ndani na Kupinda lakini tumekagua na kubaini sehemu ya juu imetitia kwa ndani, hili ni tatizo kubwa kuliko lilivyo ripotiwa awali- Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila
  • Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ileje ahakikishe waliohusika wote na ujenzi mbovu katika Hospitali ya Ileje popote pale walipo watafutwe na wachukuliwe hatua kali lakini pia Mkurugenzi ahakikishe ifikapo Juni 30, 2019 fedha zilizoletwa na serikali shilingi Bilioni 1.5 ziwe zimetumika kuendeleza ujenzi wa hospitali hiyo baada ya kurekebisha maeneo hayo yenye dosari -Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila
  • Kuna umuhimu mkubwa wa kurekebisha makossa hayo yaliyojitokeza na kuendeleza ujenzi bila kufanya hivyo kunaweza kusababisha maafa yaani jengo hili kuanguka, Makosa yaliyofanyika ni ya design ndio maana eneo lililotitia limesababishwa na uzito wake wenyewe hivyo huwezi kuendelea na ujenzi wa ghorofa hili la hospitali- Meneja wa TARURA Wilaya ya Ileje Mhandisi Lugano Mwambingu
  • Tunakiri hatukuona matatizo hayo mapema ila nia yetu ni kuhakikisha marekebisho hayo yanatekelezwa, jambo hili limetuathiri kwani nasi tulitarajia ghorofa hili likamilike ili wananchi wetu wanufaike na huduma  katika hospitali hii- Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ileje Joseph Mchome
  • Katika ziara hii pia nimebaini kuwa Kuna tatizo la serikali la vijiji kuendeshwa kwa kutofuata taratibu hasa kutofanya mikutano ya vijiji na kutotunza kumbumbuku za vijiji licha ya kuwa serikali imeajiri watendaji wenye diploma - Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila
  • Nawaagiza wakurugenzi wote Mkoa wa Songwe wafuatilie utendaji wa serikali ngazi ya vijiji, ili mapato na matumizi yabandikwe, vikao vya kisheria vifanyike na kuwepo file la mihtasari ya vikao vyote vya kijiji kwakuwa haya ni matakwa ya kisheria - Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila
  • Wajibu wa Halmashauri na waratibu wa TASAF ni kuhakikisha fedha zinawafikia walengwa na hakuna kaya hewa aidha wakaguzi wa ndani wakague fedha za TASAF kama mfuko maalumu tofauti na sasa wanavyofanya ukaguzi wa jumla ukizingatia hizi ni fedha nyingi kwani serikali kwa mkoa wa Songwe ni imetoa zaidi ya bilioni 14 kwa mpango huo- Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila
  • Halmashauri itaendelea kusimamia watendaji wa vijiji na kata ili watimize majukumu yao kisheria, tumekuwa tukiwachukulia hatua watendaji ambao hawatimizi majukumu yao na tutaendelea kufanya hivyo - Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ileje Joseph Mchome
  • Tunashukuru mpango wa TASAF kwakuwa umetukomboa kimaisha, ijapokuwa mimi ni mjane nimeweza kupata mbolea na chakula kupitia fedha za TASAF, hivyo nawashukuru sana walio anzisha mpango huu-Hana Mtawa Mkaji wa Kijiji cha Ibungu, Ileje na Mnufaika wa TASAF

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI January 30, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • SERIKALI YA SAINI MRADI WA ZAIDI YA BILIONI 119.9 UJENZI WA MRADI WA MAJI TUNDUMA VWAWA

    March 20, 2025
  • MKUU WA WILAYA YA ILEJE MHE. FARIDA MGOMI KWA NIABA YA MKUU WA MKOA AFUNGUA HUDUMA YA WIKI YA SHERIA MKOANI SONGWE

    January 25, 2025
  • TASAF MKOA WA SONGWE IMEFANYA ZIARA KUKAGUA MIRADI NA KUJIONEA UTOAJI WA HUDUMA KWA WANUFAIKA WA TASAF MOMBA

    January 03, 2025
  • KIKAO CHA TATHMINI YA HUDUMA ZA AFYA YA UZAZI NA MTOTO MKOANI SONGWE.

    November 07, 2024
  • Angalia zote

Video

ELIMU KWA WATOTO KIPINDI CHA CORONA
Video za Ziada

Kurasa za Karibu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • SALARY SLIP PORTAL
  • AJIRA

Kurasa Mashuhuri

  • IKULU
  • NECTA

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi

    Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE

    Simu: 025 2580305

    Simu ya Kiganjani: 025 2580305

    Barua pepe: ras@songwe.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Sera za Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.