RC CHONGOLO AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO WILAYANI ILEJE
HAKUNA ATAKAYEKWEPA MKONO WA DOLA KUHUSU MIMBA ZA UTOTONI - RC CHONGOLO
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe. Daniel Chongolo amekemea vikali tabia ya uwepo wa mimba za utotoni hususani wanafunzi katika Wilaya ya Ileje ambapo amesema katika utawala wake hakuna mtu yeyote atakayekwepa mkono wa dola kwa kumpatia mimba mwanafunzi.
RC Chongolo ameyasema hayo leo Aprili 28 wakati akiongea na wananchi katika ziara yake eneo la Shule ya Sekondari ya Wasichana (Ileje Girls) iliyopo kijiji cha Ikumbilo Kata ya Chitete wilayani Ileje.
"Niwaambie wala hatutaki kusema mengi ambao wao hawawezi kuacha mabinti wadogo wasome, tutawasaidia kwenda kufanya kazi nyingine zitakazofaa zaidi ili wasionane na mabinti kwa miaka 10,20,25 mpaka 30 ili wakirudi watakuwa walimu wazuri." amesema Mhe. Chongolo
Mhe. Chongolo anatarajiwa kuendelea na ziara yake kesho kukagua miradi mbalimbali ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa ziara yake ya kikazi ya siku 4 ndani ya wilaya hiyo.
|
|
|
|
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.