ZIARA YA WAZIRI MKUU MKOANI SONGWE
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa alifanya ziara ya kikazi katika Mkoa wa Songwe kuanzia tarehe 20 – 24/07/2017.
Katika ziara hiyo Waziri Mkuu alitembelea miradi mbalimbali. katika Wilaya ya Momba alitembelea mradi wa umwagiliaji wa Naming’ongo, Ujenzi wa nyumba za Watumishi na kuzindua zoezi la upimaji ardhi na kutoa Hati za Kimila. Halmashashauri ya mji wa Tunduma Mradi wa Kituo cha pamoja cha ushuru wa Forodha (One Boarder Stop Post – OSBP), Ileje alizindua ujenzi wa OPD. Kuzindua daftari la Wakazi la Kieletroniki (ambalo litatumika kuanzia ngazi ya kitongoji, na kuzindua kitabu cha Rasimu ya Mkoa wa Songwe.
Katika majumuisho alisema haya
Ulinzi na usalama
Wananchi waendelee kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama wa wananchi katika mapambano dhidi ya mauaji ya wazee, Walemavu wa ngozi – Albino, ulevi uliokithiri wa Viroba, mila zilizopitwa na wakati za kunyima haki wanawake na watoto
Pembejeo Feki
Alikemea swala la usambazaji wa pembejeo feki na kuwa serikali hitafumbia macho na alitaka ushirikiano ili kudhibiti usambazaji wa pembejeo feki
Aiongeza kuwa pembejeo zenye ubora zisambazwe kwa wakati. Uchumi
Waziri Majaliwa alisema kuwa Serikali itaendea kuwatambua na kuwaendeleza wabunifu
Uhakika wa chakula
Waziri aliwataka Wananchi wahakikishe wanakuwa na uhakika wa chakula kwa kupanga bajeti ya mavuno ili kuepukana na balaa la njaa
Upimaji wa ardhi
Wazari Mkuu alitoa shukrani kwa mkoa wa Songwe kuzingatia umuhimu wa ardhi kwa kuanza kupima ardhi yake ili iongeze thamani na kuwa na matumizi bora ya ardhi – kilimo, mifugo, hifadhi ya misitu, hifadhi ya wanyama pori na kuwa hilo litapunguza migogoro isiyo ya lazima.
Afya
Wazir Majaliwa alisisitiza umuhimu wa kuboreshewa huduma za Afya – Mama Wajawazito na Watoto
Elimu
Kutokana na serikali kutoa huduma za elimu bure Waziri aliagiza ujenzi wa shule za ufundi ili kuongeza ajira ya vijana
Vile vile kila shule ianzishe madarasa ya awali ambayo yatatumika kuwaandaa watoto wa miaka minne hadi mitano kabla ya kujiunga na darasa la kwanza.
Akijibia changamoto la uhaba wa Waalimu Waziri Majaliwa alisema serikali imetoa vibali vya ajira kwa watumishi 10,184 kuziba pengo la Watumishi Feki, na vibali vingine 52,436 ambapo katika idadi hiyo wamo Watumishi wa Sekta ya Elimu.
Utalii
Waziri mkuu aliagiza kuwa Vivutio vya utalii viboreshwe na kutangazwa ili kuongeza vyanzo vya mapato.
Ulevi
Waziri Mkuu Majaliwa alikemea tabia ya ulevi na kuzuia usambazaji na matumizi ya pombe aina ya Viloba.
Hali ya ulinzi na Usalama mipakani
Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa alitoa agizo kuwa waliojenga nyumba ndani ya mita 50 kutoka mpaka wa Tanzania na Zambia wabomoe wenyewe katika muda wa siku.
Akiongea kwenye mkutano wa hadhara baada ya kutembelea mpaka huo aliagiza Halmashauri kuweka alama kwenye nyumba 250 ambazo zilibainika kuwa ndani ya eneo huru (No man’s land) zinatakiwa kubomolewa kwa muda usiozidi miezi mitatu.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.