• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
SONGWE REGION
SONGWE REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa MKOA WA SONGWE

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Sehemu
      • Mipango na Uratibu
      • Idara ya Elimu
      • Huduma za Maji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Huduma za Serikali za Mitaa
      • Miundombinu
    • Vitengo
      • Huduma za Kisheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
  • Wilaya
    • Mbozi DC
    • Songwe DC
    • Momba DC
    • Ileje DC
  • Halmashauri
    • Mbozi
    • Ileje
    • Momba
    • Songwe
    • Tunduma
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Mifugo
    • Madini
    • Kilimo
    • Biashara
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya na Ustawi Wa Jamii
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma ya Mifugo na Uvuvi
    • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
    • Mipango na Takwimu
    • Ujenzi
  • Machapisho
    • Sheria
    • Miongozo
    • Sera
    • Fomu za Maombi
    • Utaratibu
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

ZIARA YA WAZIRI WA NCHI OR TAMISEMI SULEIMAN JAFFO MKOANI SONGWE NOVEMBA 26, 2018

Posted on: November 27th, 2018

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Suleiman S. Jaffo amefanya ziara ya siku moja katika halmashauri tatu za Mkoa wa Sogwe ambazo ni Songwe, Mbozi na Tunduma. Katika ziara hiyo amekagua miradi mbalimbali na kuzungumza na watumishi katika halmashauri zote tatu. Yafuatayo ni baadhi ya yaliyojiri katika ziara yake;

  1. Mkoa wa Songwe unao upungufu wa watumishi kwa asilimia 40, wataalamu wa kusimamia ujenzi wa miradi mbalimbali pia ni wachache, aidha tunalo tatizo la baadhi ya watumishi kutokuwa waadilifu na baadhi tumesha wachukulia hatua- Brig. Jen. (Mst) Nicodemus Mwangela.
  2. Tunafahamu Mkoa mpya unakuwa na matatizo na changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na upungufu wa watumishi, ubovu wa miundombinu na vitendea kazi, OR TAMISEMI itatoa kipaumbele kwa mkoa wa Songwe katika mgao wa watumishi na magari kwa ajili ya viongozi -  Waziri Jaffo.
  3. Tunafahamu lipo tatizo la mahusiano mabaya kati ya viongozi mbalimbali katika halmashauri za Mkoa wa Songwe, ila nimefarijika kuwa Mkuu wa Mkoa na Katibu Tawala Mkoa waliopo sasa wameonyesha kuwa ni viongozi wa kutatua matatizo ya watu- Waziri Jaffo.
  4. Mkuu wa Mkoa wa Songwe ahakikishe TBA wanasimamia majengo yote waliyopewa kuyasimamia, endapo watashindwa au kucheleweshwa Mikataba ya kazi hizo ivunjwe na wapewe taasisi nyingine za serikali kazi ya kusimamia ujenzi wa miradi hiyo ili ikamilike haraka- Waziri Jaffo.
  5. Naagiza miradi mipya yoyote  ya ujenzi kuanzia sasa akipewa Suma JKT msimamizi asipewe TBA kwakuwa utaleta mgongano wa kimaslahi, kazi ya usimamizi wapewe taasisi nyingine kama vile Mbeya University au Ardhi University, Waziri Jaffo.
  6. Utendaji kazi wa mweka hazina utaweza kuikwamisha au kuiendeleza halmashuri, maafisa manunuzi pia wana kazi kubwa ya kufanya, Wakurugenzi watumieni maafisa maendeleo ya jamii kufanikisha mikopo kwa vijana, wanawake na walemavu, pia kuhakikisha jamii ijiunge na mifuko ya bima ya afya (CHF), kwa bahati mbaya maafisa Maendeleo ya jamii hawatumiki kabisa- Waziri Jaffo.
  7. Kuna tabia ya upendeleo, baadhi ya wakuu wa idara wana upendeleo wa maafisa Fulani walio chini yao, utakuta semina zote anaenda mtu mmoja tu, pia maafisa utumishi waache upendeleo, michakato ya kupanda madaraja yanaanzia ofisi ya utumishi katika halmashauri, hivyo nawasihi mfanye kazi kwa ushirikiano- Waziri Jaffo.
  8. Pongezi kwa ujenzi mzuri wa vituo vya afya vya Mbuyuni, Isansa na Tunduma, Serikali itaongeza vituo vingine vya Afya katika halmashauri za Songwe na Mbozi, aidha ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Songwe uanze mara moja kwa fedha zilizo kwisha tolewa sh milioni 500, fedha nyingine zaidi ya bilioni moja zitaletwa- Waziri Jaffo.
  9. Wataalamu wetu wa TARURA na TANROADS wataangalia namna ya kuiunganisha wilaya ya Songwe na Makao makuu ya mkoa wa Songwe bila ya kuzungukia Mkoa wa Mbeya kama ilivyo sasa, tuna kila sababu ya kujenga barabara hilo na serikali itahakikisha hilo linafanikiwa- Waziri Jaffo.
  10. Mkuu wa Mkoa wa Songwe afanye ufuatiliaji kuhusu viongozi waliojingiiza katika biashara na hawafuati sheria mfano biashara ya madini, Kiongozi yeyote anaruhusiwa kufanya biashara isipokuwa biashara hiyo isilete mgongano  wa kimaslahi na cheo chake pia afuate sheria, kanuni na taratibu za nchi- Waziri Jaffo.
  11. Watumishi wa umma fanyeni kazi kwa bidi, hakikisheni utumishi wenu unaacha alama nzuri, sio ukihama watu wanabaki wanafurahia au ukiwa likizo hakuna wa kukuulizia, mpewa dhamana kubwa ya kuwatumikia wananchi-Waziri Jaffo.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI January 30, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • SERIKALI YA SAINI MRADI WA ZAIDI YA BILIONI 119.9 UJENZI WA MRADI WA MAJI TUNDUMA VWAWA

    March 20, 2025
  • MKUU WA WILAYA YA ILEJE MHE. FARIDA MGOMI KWA NIABA YA MKUU WA MKOA AFUNGUA HUDUMA YA WIKI YA SHERIA MKOANI SONGWE

    January 25, 2025
  • TASAF MKOA WA SONGWE IMEFANYA ZIARA KUKAGUA MIRADI NA KUJIONEA UTOAJI WA HUDUMA KWA WANUFAIKA WA TASAF MOMBA

    January 03, 2025
  • KIKAO CHA TATHMINI YA HUDUMA ZA AFYA YA UZAZI NA MTOTO MKOANI SONGWE.

    November 07, 2024
  • Angalia zote

Video

ELIMU KWA WATOTO KIPINDI CHA CORONA
Video za Ziada

Kurasa za Karibu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • SALARY SLIP PORTAL
  • AJIRA

Kurasa Mashuhuri

  • IKULU
  • NECTA

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi

    Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE

    Simu: 025 2580305

    Simu ya Kiganjani: 025 2580305

    Barua pepe: ras@songwe.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Sera za Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.