HISTORIA.
Tafiti zinaonesha kuwa hakuna mwenyeji wa Wilaya ya Ileje. Wakazi wa Ileje wamehamia kutoka sehemu mbalimbali za Rungwe, Mbeya Vijjini, Zambia, Malawi na Afrika kusini. Kuna makabila makuu matatu yakiongozwa na Wandali, Walambya ambao wapo katika nchi ya Tanzania na Malawi, Wamalila, na makabila madogo ya Waiga, Wanyiha na Wanyamwanga.
UTATUZI WA MIGOGORO
Wandali wanapinga na kushughulikia uharibifu wa mazingiara, mauji ya Wazee na Walemavu, vitendo vya ushirikina na Wizi wa aina yoyote ile.
Tatizo la mtuhumiwa yeyote linachukuliwa ni tatizo la ukoo mzima na utatuzi huhusisha ukoo wake.
HIFADHI YA MAZINGIRA
Wandali wanaishi katika sura ya nchi iliyo katika miinuko na mabonde yenye hali yenye ubaridi na ubichi mwaka mzima hivyo kuwafanya wafanye kazi za kilimo kwa mwaka mzima. Hali hiyo inaruhusu uwepo wa miti mingi ya asili na ya kupanda. Jamii hii hutumia misitu kwa ajili ya matambiko, kupata dawa za asili, kupata matunda na mbao. Ni manufaa haya ambayo yanawafanya wazuie watu wasikate miti ovyo.
SHUGHULI ZA KIUCHUMI.
Wandali ni Wakulima, Wafugaji, Wahunzi na Wasukaji. Katika kilimo wanalima Mahindi, Ndizi, Ulezi, Magimbi, Viazi na Jamii ya mikunde kama Kunde, Maharage, kutengeneza bidhaa zinazotokana na mianzi.; Wanafuga ng’ombe, Mbuzi, Kondoo, na Kuku; Wahunzi wanatengeneza zana za matumizi ya nyumbani kama shoka, Nyengo na Silaha kama Mikuki na mishale.
Vilevile wanatengeneza bidhaa mbalimbali zinazokana na mianzi kama Nyungo, Viti, Meza, na mapambo mbalimbali.
Wandali wanasifiwa kwa uwezo wao wa kufanya kazi kwa bidii kama kilimo, na biashara.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.