RAS DKT HAWASSI AONGOZA KIKAO CHA TATHMINI YA MIUNDOMBINU YA ELIMU
Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe, Dkt. Frank Hawassi, leo tarehe 13 Februari 2026, ameongoza kikao cha tathmini ya miundombinu ya elimu mkoani humo.
Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe, kikihusisha maafisa elimu wa wilaya, wakurugenzi wa halmashauri pamoja na wadhibiti ubora wa shule.
Akizungumza katika kikao hicho, Dkt. Hawassi alisisitiza umuhimu wa kuboresha miundombinu ya elimu ili kuhakikisha mazingira bora ya kujifunzia na kufundishia, sambamba na kuongeza ubora wa elimu kwa wanafunzi.
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
Aidha, aliwataka wadau wa sekta ya elimu kushirikiana kwa karibu katika kutekeleza mipango ya maendeleo, hususan katika ujenzi, ukarabati na matengenezo ya miundombinu ya shule.
Kikao hicho kimekuwa sehemu ya juhudi za Mkoa wa Songwe katika kuimarisha sekta ya elimu na kufikia malengo ya maendeleo endelevu.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.