Sekta ya Mifugo ni mojawapo ya shughuli kuu za kiuchumi inayotegemewa na wananchi wa Mkoa wa Songwe. Mkoa unajitosheleza kwa mahitaji ya nyama na kiasi kikubwa cha mifugo husafirishwa kwenda nje ya mkoa.
JEDWALI NA: IDADI YA MIFUGO NDANI YA MKOA.
Mnyama
|
Halmashauri |
Jumla
|
||||
|
Ileje
|
Mbozi
|
Momba
|
Tunduma
|
Songwe
|
|
Ng’ombe asili
|
39602 |
107681 |
11,8027 |
5265 |
123,756 |
394,331 |
Ng’ombe maziwa
|
3392 |
6752 |
401 |
92 |
105 |
10742 |
Mbuzi
|
32545 |
61,781 |
73,497 |
615 |
72,955 |
241,393 |
Kondoo
|
3,757 |
5,256 |
9,884 |
97 |
13,305 |
32,299 |
Nguruwe
|
6396 |
23,343 |
8067 |
2332 |
33,046 |
73,184 |
Kuku asili
|
148,809 |
560,925 |
155,233 |
39289 |
153,695 |
1,057,951 |
Kuku kisasa
|
571 |
2,550 |
10,351 |
9136 |
- |
22,608 |
Bata
|
- |
3,860 |
5,096 |
216 |
- |
9,172 |
Punda
|
16 |
722 |
1,547 |
39 |
1,174 |
3,498 |
Chanzo: Halmashauri za Wilaya, 2017
BORESHAJI WA MIFUGO.
Mkoa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa ufugaji umeendelea kuboresha mifugo ili kuongeza uzalishaji wenye tija hasa kwa ng’ombe wa maziwa, kuku pamoja na nguruwe. Mifugo hii imekuwa ikinunuliwa kupitia miradi mbalimbali ikiwa ni pamoja na ASDP/DADPS, ACGG na Heifer International ambapo Mradi wa Heifer umenunua ng’ombe 200 kwa wafugaji wa kata za Isansa na Igamba katika Wilaya ya Mbozi na wamesambazwa kwa wafugaji.
MAGONJWA YA MIFUGO.
Mkoa unakumbwa na magonjwa yanayoenezwa na kupe, chambavu, kuharisha, mapere ngozi, kichaa cha mbwa, minyoo, ukurutu na homa ya nguruwe.
KUTENGA MAENEO.
Eneo lililotengwa kwa ajili ya mifugo ni hekta 261,516.18 kwa ajili ya malisho katika Wilaya za Momba na Songwe. Katika Wilaya ya Momba vijiji vilivyotenga maeneo ya malisho ni 20 na Songwe ni vijiji 8
HALI YA UTAMBUZI, USAJILI NA UFUATILIAJI WA MIFUGO.
Zoezi la Utambuzi na Usajili kwa kupiga chapa katika Mkoa lilichelewa kuanza kutokana na ufinyu wa bajeti ambapo ilipelekea hali ya uhamasishaji kuchukua muda mrefu. Zoezi limeanza mwezi Oktoba ambapo lilizinduliwa Rasmi tarehe 17 Oktoba 2017 na Mhe. Mkuu wa Mkoa katika Wilaya ya Songwe. Hadi kufikia tarehe 02 Disemba 2017 Jumla ya ng’ombe 94991 (Ileje 18282, Mbozi 43779, Songwe 28,173 na Tunduma 4757) wamepigwa chapa .
Uhimilishaji
Mkoa wa Songwe uhimilishaji unaendelea katika Halmashauri ya Mbozi. Ng’ombe 474 wamehilimishwa kipindi cha Januari 2017 - Septemba 2017 kati ya lengo la ng’ombe 500 kwa mwaka.
Nyama
Mkoa umezalisha kilo za nyama 2,326,832 katika kipindi cha Januari 2017 – Septemba 2017.
Maziwa
Jumla ya lita 14,136,400 zenye thamani ya Sh. 9,895,480,000 zimezalishwa kwa kipindi cha januari 2017 mpaka Septemba 2017 kwa ujumla kutoka ng’ombe wa aina zote na mbuzi.
Ngozi
Uzalishaji wa ngozi ni wa shida kutokana na kutokuwepo kwa bei nzuri na soko la uhakika. Kipindi cha Januari 2017 - Septemba 2017 vipande vya ngozi 9,740 vya ng’ombe, vipande 7,842 vya mbuzi na kondoo vipande 3,694 vilikusanywa.
Mauzo ya Mifugo
Mkoa una jumla ya minada 7 inayofanya kazi katika Halmashauri za Wilaya Ileje, Mbozi, Momba na Songwe. Kipindi cha Julai 2017 - September 2017 jumla ya ng’ombe 2,854 wenye thamani ya Sh. 1,926,450,000. waliuzwa, mbuzi na kondoo 2,461 wenye thamani ya Sh. 147,660,000.00 waliuzwa.
Miundo mbinu ya mifugo
Malambo
Mkoa una lambo moja katika kijiji cha Kasanu Wilaya ya Momba kwa ajili ya kunyweshea mifugo. Ujenzi wa lambo katika kijiji cha Mkomba Wilaya ya Momba unaendelea na ujenzi wa bwawa la Mbangala katika Wilaya ya Songwe unaendelea na linajengwa na Wakala wa Mabwawa na Visima (DDCA) kwa fedha za Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa gharama ya Sh. 2,400,000,000.00
Machinjio na makaro
Mkoa una machinjio makubwa 8 na makaro 37. Machinjio na makaro haya yanatumika katika kuchinjia ng’ombe, mbuzi kondoo na nguruwe. Ambapo ng’ombe, mbuzi na Kondoo hutumia kwa pamoja isipokuwa machinjio ya nguruwe hujitegemea.
Jedwali. Na. 17 Machinjio yaliyopo katika Mkoa wa Songwe
Halmashauri
|
Mbozi
|
Momba
|
Ileje
|
Tunduma
|
Songwe
|
Jumla
|
Machinjio
|
2 |
1 |
2 |
1 |
2 |
8 |
Makaro
|
10 |
8 |
4 |
2 |
13 |
37 |
Hali ya majosho
Mkoa una majosho 7 kati ya hayo 2 ni mazima na yanafanya kazi, Majosho 5 hayafanyi kazi kwa sababu ya ukosefu wa maji, kuingiliwa na wakulima kwa kulima kwenye njia za kwenda kwenye majosho na ujenzi wa makazi. Mkakati wa kukabiliana na hali hiyo umewekwa kwa kusisitiza na kuhimiza wafugaji kuogesha kwa kunyunyizia na zaidi kuzingatia chanjo ya ndigana kali.
Miundombinu mingine
Mkoa katika Wilaya ya Mbozi ina mitambo ya Biogas 127 na kati ya hiyo mitambo 117 inafanya kazi.
Afya ya mifugo
Mkoa una vituo viwili vya kutolea huduma za mifugo (LDC’s), kimoja kipo Halmashauri ya Ileje na kingine Halmashauri ya Mbozi. Sehemu kubwa ya huduma hutolewa katika maeneo ya wafugaji pale wataalam wanapowatembelea au kuitwa na wafugaji.
Magonjwa ya mifugo na matibabu yake
Magonjwa ya Mifugo yanayojitokeza sana katika Mkoa wa Songwe ni magonjwa yanayoenezwa na kupe, chambavu, kuharisha, mapere ngozi, kichaa cha mbwa, minyoo, ukurutu na homa ya nguruwe. Magonjwa ya kuku ni mdondo, homa za matumbo na ndui
Maduka ya nyama
Mkoa una maduka ya nyama 84 katika Halmashauri zake tano.
Maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya mifugo
Eneo lililotengwa kwa ajili ya mifugo ni hekta 261,516.18 kwa ajili ya malisho katika Wilaya za Momba na Songwe. Katika Wilaya ya Momba vijiji vilivyotenga maeneo ya malisho ni 20 Songwe ni vijiji 8.
Miradi ya mifugo
Miradi ambayo inaendesha shughuli za kuwasaidia wafugaji katika Mkoa wa Songwe ni Heifer International (T), East Africa Dairy Development II na East Africa Dairy Genetic Gain. Miradi hii inasaidia kuinua sekta ya Mifugo
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.