SEKTA YA UVUVI
Uzalishaji wa Samaki
Katika msimu wa mwaka 2016/2017 tani 103.37 za thamani ya Sh. 465,165,000.00 zilizalishwa kwenye maziwa, malambo na mito ya asili. Sehemu kubwa ya uzalishaji huu umechangiwa na ziwa Rukwa, sehemu ndogo kuchangiwa na mabwawa ya taasisi, vikundi na watu binafsi.
Kudhibiti Uvuvi Haramu
Mkoa unafanya doria mara kwa mara pamoja na usimamizi shirikishi kwa kuanzisha Kamati za Usimamizi (BMUs) tano ambazo zimesajiliwa kisheria zilizopo mwambao mwa Ziwa Rukwa ili kusimamia rasilimali za Uvuvi, mazingira na Uvuvi haramu ambapo makokoro 87 yenye thamani ya Sh. milioni 9.2 yalikamatwa, nyavu 13 zenye thamani ya Sh. milioni 6 zilikamatwa na mitumbwi 60 baada ya wavuvi kukimbia, pia elimu inaendelea kutolewa kwa wananchi juu ya ufugaji bora wa samaki katika mabwawa ambapo Mkoa una jumla ya mabwawa 383 .
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.