AFISA MIPANGO NA MGANGA MKUU WASIMAMISHWA KWA MATUMIZI YA FEDHA MILIONI 800 BILA MUONGOZOILEJE:
Mkuu wa mkoa wa Songwe Omary Mgumba amemuagiza katibu Tawala wa mkoa, Ndg. Missaile Musa huo kuwasimamisha kazi na kuwachukulia hatua za kinidhamu afisa mipango na mganga mkuu wa halmashauri ya Ileje Kwa kudanganya kutokuwa na mwongozo wa matumizi ya fedha milioni 800 zilizoletwa na Serikali kwa ajili ya uboreshaji wa Hospitali ya Wilaya ya Ileje.Mgumba amefikia maamuzi hayo wakati wa ukaguzi wa mradi wa maendeleo ikiwepo ujenzi wa jengo la wagonjwa mahututi ICU huku wakidai hawana mwongozo kutoka serikaliniMgumba amesema muongozo unataka milioni 800 zijenge chumba cha kuhifadhi maiti, wodi mbili ya wanaume na wanawake kwa ajili ya kulaza wagonjwa waliofanyiwa upasuaji na chumba cha upasuaji.Mgumba ameshangazwa na uongozi wa Hospitali kuanza kujenga ukuta wa kuzunguka Hospitali, njia za kupitia wagonjwa (walk way) na kufanya ukarabati wa jengo la wagonjwa wa nje OPD kinyume na muongozo uliopo."Hata kwenye nyumba zetu binafsi uwezi kuanza na kujenga ukuta wakati nyumba ya kuishi haijaisha" Mhe. Omary Mgumba.Afisa mipango na Mganga mkuu wa halmashauri ya Ileje waliopoulizwa wanajenga kwa kufuata muongozo upi wao walisema hawajawai pata muongozo.Kufuatia hatua hiyo, Mkuu wa Mkoa ameiagiza TAKUKURU Ileje kufanya uchunguzi wa kina kama kuna njia hovyo yeyote ambayo watumishi hao walitaka kuifanya dhidi ya mradi wa Hospitali ya Ileje.Wakati huo huo, Mkuu wa Mkoa ameagiza ujenzi wa wodi mbili pamoja na jengo la kuhifadhi maiti uanze mara moja kama muongozo unavyotaka pamoja na kuendelea na ukamilishaji wa jengo la wagonjwa wa nje kwa fedha iliyobaki kiasi cha milioni 500."Kwa sababu hapa kuna jengo la upasuaji ni vyema kuanza kujenga majengo yaliyotakiwa kujengwa na kusitisha ujenzi wa uzio mpaka pale majengo muhimu ya kutolea huduma yatakapokamilika" Mhe. Omary Mgumba.Mkuu wa Mkoa anaendelea na ziara yake ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo na kuongea na wananchi kusikiliza kero.MWISHO.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.