BWAWA LA MUKO LA BILIONI 1.9 KUHUDUMIA WANANCHI 11,671, MIFUGO 3,430.
MOMBA: Serikali imekamilisha ujenzi wa bwawa la muko lililopo kijiji cha Mengo Halmashauri ya Wilaya ya Momba lenye uwezo wa kuhifadhi maji lita milioni 166,386,474 ambalo limegharamia shilingi Bilioni 1,991,509,182.55.
Mhandisi Jackson Waledi kutoka Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Rukwa amesema bwawa la Mengo litahudumia wananchi wapatao 11,671 pamoja na mifugo ipatayo 3,430.
Mhandisi Jackson Waledi amesema kulingana na usanifu uliofanyika maji yatakuwa yanatumika kwa mwaka mzima kwa kipindi cha miaka 50 ijayo kuanzia kiangazi hadi masika wananchi wanaozunguka Bwawa ili watanufaika
"Kwa sasa bwawa la Muko limekabidhiwa kwa RUWASA ili waweze kujenga sehemu ya kutibu maji kwa ajili kuwasambazia wananchi maji" Eng. Waledi.
Pia, Mhandisi Jackson Waledi amesema Bwawa la Muko kuna sehemu maalumu iliyojengwa kwa ajili ya kuhudumia mifugo ipatayo 3,430 ya wakazi wa Mengo na vijiji jiran
Ephrahim Swila mkazi wa kijiji cha Mengo pamoja na kuishukuru Serikali kwa Bwawa la Muko ameiomba Serikali kuimarisha ulinzi kwa kuweka uzio kwenye bwawa lote.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Dkt. Francis Michael amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan inawajali wananchi hivyo ni jukumu la kila mwananchi kuweza kulinda mradi huu kwa kuepuka kufanya shughuli za kibinadamu kwenye Bwawa.
"Tusioshe vyombo, tusifue nguo hapa, wala kuogea hapa kwani kufanya hivyo ni kuchafua maji ambayo tunategemea ya wahudumiwe wananchi" Mhe. Dkt. Francis Michael.
Mkuu wa Mkoa, Mhe. Dkt. Francis Michael amesema mradi wa Bwawa la Muko unaenda kuongeza wigo wa upatikanaji wa maji safi na salama kwa wakazi wa Kata ya Ikana.
MWISHO.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.