Dkt. SHEKALAGHE AZITAKA HALMASHAURI KUTENGA PESA YA UJENZI WA MADARASA KILA MWAKA.
Katika kutatua changamoto ya ujenzi wa vyumba vya madarasa mwishoni mwa mwaka, Katibu Tawala Mkoa, Dkt. Self Shekalaghe amezitaka Halmashauri za Songwe kutenga fedha za ujenzi wa madarasa zitakazo onyesha idadi ya vyumba wanavyojenga kila mwaka wa fedha kutoka kwenye mapato ya ndani.
"Nataka kuanzia Januari 2021 kila Halmashauri ionyeshe imetenga fedha kiasi gani kutoka kwenye mapato ya ndani ambazo zitakwenda kujenga madarasa kwa ajili ya mwaka 2022" Katibu Tawala Mkoa, Dkt. Self Shekalaghe. 18 Disemba 2020.
Dkt. Shekalaghe amesema mkakati wa ujenzi wa madarasa kwa wanafunzi 2022 unatakiwa kuanza sasa na unapaswa kuwa endelevu kila mwaka kwa sababu Takwimu za maoteo tunazo na tunajua ni wanafunzi wangapi ambao watahitimu Darasa la Saba.
Upungufu wa vyumba vya madarasa kwa Mkoa ni vyumba 37 ambavyo vyote viko katika hatua mbalimbali za ukamilishaji na ifikapo Januari 2021 Wanafunzi wa kidato cha kwanza watavitumia.
Wanafunzi wote waliofaulu kwa Mkoa wa Songwe wamepangiwa Shule na maandalizi ya kuwapokea yanaendelea.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.