Dkt. SHEKALAGHE VYUO VYA UFUNDI NA VIKUNDI VYA UJASILIAMALI MBADALA KWA WANAFUNZI AMBAO HAWAJAFAULU
Katibu Tawala Mkoa wa Songwe, Dkt. Self Shekalaghe amesema kuanzisha kwa vikundi vya ujasiliamali na vyuo vya ufundi kwenye Halmashauri ni mbadala kwa wanafunzi ambao hawajafaulu kwenda Sekondarii.
Katibu Tawala amesema ayo wakati wa kutangaza majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kwa 2021 na kubaini wanafunzi wapatao 11,558 hawajulikani walipo.
Dkt. Shekalaghe amesema wanafunzi waliomaliza Darasa la saba 2020 wakati wanajiunga Darasa la kwanza 2013 walikuwa 29,835 lakini wanafunzi 6,136 hawakufika Darasa la saba.
Aidha wanafunzi 23,696 walisajiliwa Darasa la saba 2020 na walikuwa tayari kufanya Mtihani lakini waliofanya mtihani walikuwa 23,158 na 541 hawakufanikiwa kufanya Mtihani.
Wakati huhuo kwa wanafunzi 23,158 waliofanya Mtihani ni wanafunzi 18,277 ndio waliofaulu na 4,881 hawajafaulu.
"Ukijumlisha 541 ambao hawakufanya Mtihani, 6,136 ambao walidondoka hawakufika darasa la saba na hawa 4,881 ambao hawajafaulu unapata wanafunzi 11,558 ambao kama Mkoa hatujui wako wapi" Dkt. Shekalaghe.
Dkt. Shekalaghe ametoa wito kwa Halmashauri kutumia vizuri Chuo cha ufundi stadi VETA cha Ileje na Myunga cha Momba kuhamasisha Wazazi/walezi kupeleka wanafunzi, kwani Mwanafunzi akitoka VETA atakuwa msaada kwa jamii na Taifa.
"Kwa ili la VETA kila Halmashauri ione umhimu wa kuwa na Chuo cha VETA kwake kwa kuanza na fani za kawaida kwanza" Dkt. Shekalaghe.
Pia, Dkt. Shekalaghe amezitaka Halmashauri kusimamia mikopo ya vijana kwa ajili ya vikundi vya ujasiliamali.
Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Mhe. Joseph Mkude amesema Chuo cha VETA Serikali imewekeza fedha zaidi Bilioni 1 na kina madarasa, mabweni na vifaa vya kujifunzia lakini wanafunzi wapo 24 tu, tukitumie vizuri Chuo iki Wazazi/walezi kutoka Halmashauri zote za Mkoa tukitumie vizuri kwa ajili ya wanafunzi ambao hawajabahatika kufaulu.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.