ELIMU YA UNAWAJI MIKONO IONGEZEKE KUJIKINGA MAGONJWA YA MLIPUKO.
SONGWE: Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Waziri Kindamba ametoa rai kwa viongozi wa Afya Mkoa na katika Halmashauri zote za mkoa wa Songwe kuongeza kasi ya kutoa Elimu ya unawaji mikono ili kujikinga na magonjwa ya tumbo na magonjwa mengine ya mlipuko ambayo yana uathiri mkoa.
Mkuu wa Mkoa, Mhe. Waziri Kindamba amesema hayo leo Oktoba 15, 2022 katika maadhimisho ya siku ya unawaji mikono Dunia ambayo kimkoa yamefanyika katika kijiji cha Mbozi kata ya Igamba wilayani Mbozi.
Mhe. Kindamba amesema Mkoa wa Songwe haufanyi vizuri katika suala la unawaji mikono, uharibifu wa mazingira na ujenzi wa vyoo bora, hivyo kuwa kwenye hatari ya kupata magonjwa ya tumbo na milipuko kama vile kipindupindu, UVIKO-19 na Ebola.
‘’Tunashika nafasi ya 17 kitaifa katika suala zima la unawaji mikono , ambapo kaya zenye vifaa vya kunawa mikono katika vyoo ni 35%, wakati wastani wa unawaji mikono kitaifa ni 41% Mikoa mitatu inyoongoza kwa kuwa navifaa vya kunawia mikono ni Iringa 77%, Njombe 73.9% na Kilimanjaro 73.5%“ Mhe. Waziri Kindamba.
Mkuu wa Mkoa, Mhe. Waziri Kindamba amesema Halmashauri ya mji Tunduma ipo chini kwa 17%, Songwe 27%, Mbozi 36%, Ileje 39% na Halmashauri ya Momba 44% kutokana na takwimu izi mkoa una kazi kubwa ya kufanya kwa viongozi wakishirikiana na wananchi katika Halmashauri kuwa na mipango ya kuhakikisha tunakuwa na vyoo bora sambamba na vifaa vya kunawia mikono katika kaya , shule na maeneo mbalimbali zinapofanyika shughuli za maisha.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Songwe Dkt. Boniface Kasululu amesema malengo ya mkoa ni kuongeza kiwango cha kaya zenye vyoo bora kutoka 78% hadi kufikia 100% na kuongeza kiwango cha kaya zenye vifaa vya kunawa mikono kutoka 35% hadi kufikia 50% ifikapo Disemba 2023.
Kwa upande wake Afisa mabadiliko tabia ya jamii kutoka taasisi isiyo ya kiserikali ya Tanzania Communication and Development Center (TCDC) Gaston Gration amesema kuwa magonjwa mengi ya tumbo na kuhara wanayo umwa wanachi wa Songwe yanatokana na uchafu wa kuto kunawa mikono sambamba na uchafu na uharibifu wa mazingira.
MWISHO.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.