EWURA YAWASILISHA UTENDAJI KAZI WA MAMLAKA ZA MAJI
SONGWE: Mamlaka ya udhibiti wa huduma za Nishati na Maji (EWURA) imewasilisha taarifa ya mwenendo wa utendaji wa Mamlaka za maji na usafi wa Mazingira za Vwawa-Mlowo na Tunduma kwa timu ya watalamu wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe kwa ajili ya kutoa mapendekezo ya namna ya kuboresha huduma kwa mamlaka za maji.
EWURA ina wajibu wa kufatilia utendaji wa Mamlaka za maji nchini kwa mujibu wa sheria ya maji na usafi wa Mazingira 2019 kifungu. 29(1).
Katibu Tawala Mkoa wa Songwe, Bi. Happiness Seneda amewapongeza EWURA kwa taarifa iliyoonyesha hali halisi ya utendaji pamoja na mapendekezo ya kuboresha utendaji kazi wa Mamlaka za Vwawa-Mlowo na Tunduma.
MWISHO
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.