HAKIKISHENI KAYA ZOTE ZINAHESABIWA, RAS SENEDA.
SONGWE: Katibu Tawala Mkoa wa Songwe, Bi. Happiness Seneda amewataka viongozi ngazi ya kitongoji, kijiji na Kata kuhakikisha kaya zote zinahesabiwa zilizopo kwenye maeneo yao.
Katibu Tawala Mkoa ametoa wito huo wakati akiongea na waandishi wa Habari kutoa tathimini ya zoezi la Sensa ya watu na makazi linavyokwenda ndani ya Mkoa wa Songwe.
Bi. Happiness Seneda amewataka waheshimiwa Madiwani, wenyeviti wa vijiji kila moja kwenye eneo lake ahakikishe kaya zote zimehesabiwa kwenye eneo lake.
Tumeona zoezi la Sensa katika Mkoa wa Songwe linaendelea vizuri katika maeneo mengi ni wajibu wetu viongozi wote kuhakikisha kila kaya kwenye eneo unalosimamia imehesabiwa, amesema Bi. Happiness Seneda.
Pia, Katibu Tawala Mkoa wa Songwe, Bi. Happiness Seneda ametoa wito kwa wananchi wote ambao bado hawajahesabiwa kuhakikisha wanahesabiwa kwa maendeleo ya Taifa.
Aidha, kwa sasa Serikali imeongeza makarani sehemu ambazo kuna kaya nyingi hazijahesabiwa ili kuhakikisha kila kaya inahesabiwa.
Nitoe wito kwa wananchi kuacha taarifa muhimu kwenye kaya zao pamoja na namba ya simu ili makarani waweze kufanya kazi kwa ufasihihi, Bi. Happiness Seneda.
Sensa ya watu na makazi inaendeleea kwa wananchi ambao bado hawajahesabiwa.
MWISHO.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.