ILEJE YATATUA KERO YA WANAFUNZI KUFUATA MASOMO UMBALI WA KM 14.ILEJE: Wanafunzi wanaotoka kijiji cha Shinji na Mtima sasa hawatatembea umbali wa KM 14 kwenda na kurudi kufuata masomo yao katika Sekondari ya Mbebe, baada ya Serikali kutatua kero yao kwa kujenga Shule mpya ya Sekondari katika Kijiji cha Shinji.Shule hiyo imekamilika baada ya uongozi wa Ileje kuhamisha pesa Milioni 80 za Mpango wa maendeleo kwa Ustawi Taifa na mapambano dhidi ya UVIKO ambazo zilitakiwa kujenga vyumba vya madarasa kwenye Shule ambazo hazina mahitaji, ndio Uongozi ukaamua kujenga katika kijiji cha Shinji ili kuwapunguzia kero wanafunzi.Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Omary Mgumba amewapongeza wana Shinji na Uongozi wa Ileje kwa busara zao za kuamua kutatua kero kwa kuamua kujenga Shule sehemu zenye mahitaji.Mkuu wa Mkoa amefanya ukaguzi wa Shule baada ya Kukamilika, ikumbukwe Mhe. Omary Mgumba alishiriki ujenzi wa Shule hii katika hatua ya msingi Disemba 2021.MWISHO.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.