JAMII ISHIRIKISHWE KUWAFIKIA WATOTO WASIOPATA CHANJO YA SURUA. Dkt. KASULULU.
SONGWE: Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe, Dkt. Boniface Kasululu ametoa wito kwa timu za usimamizi wa huduma za Afya ngazi ya Halmashauri na Mkoa kuwatumia vizuri viongozi ngazi ya jamii ili kuwafikia watoto wote wenye umri chini ya miaka ya mitano ambao hawajapata chanjo ya surua Rubella dhidi ya ugonjwa wa Surua.
Dkt. Kasululu ametoa wito huo kwenye kikao kazi cha tathinini ya zoezi la utoaji wa chanjo kwa watoto wa umri chini ya miaka mitano kufuatia zoezi la chanjo lililofanyika 29 Machi hadi Aprili 2 kwa lengo la kuwatambua watoto wasiopata chanjo na wale ambao hawakumaliza chanjo mbalimbali.
"Viongozi wa kitongoji tukiwashirikisha wao wanazijua vizuri kaya ambazo zina watoto wa umri chini ya miaka mitano na kwa kufanya hivyo tutakuwa tunawafikia watoto wengi zaidi kwa wale wasiopata na wasiomaliza chanjo" Dkt. Boniface Kasululu Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa.
Pia, Dkt. Kasululu ameziagiza Timu za usimamizi wa huduma za Afya Mkoa na Halmashauri kutumia takwimu vizuri walizonazo pale wanapokwenda kuwafutilia watoto ambao hawajapata au kutomaliza chanjo.
Tunajua tuna mfumo mzuri wa kuweka kumbukumbu zetu vizuri kuanzia pale mtoto anapozaliwa hadi kwenye mahudhurio ya kliniki na watoto wote tunajua wanatoka mtaa, kitongoji gani sasa tuende tukatunie vizuri takwimu izi kwa kushirikiana na jamii kuwafikia watoto wasiomaliza chanjo na wale wasiopata kabisa, amesisitiza Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe, Dkt. Boniface Kasululu.
Mratibu wa chanjo Mkoa wa Songwe, Moses Lyimo amesema zoezi la utoaji wa chanjo kwa watoto ni endelevu watahakikisha wanawafikia watoto wote ambao hawajapata chanjo ya Surua Rubella lakini kwa wakati huo huo watalamu watamfuatilia mtoto kama amepata chanjo nyingine kama vile Polio, Penta na wakimkuta mtoto mojawapo hakupata chanjo hiyo basi atapatiwa hapo hapo.
MWISHO.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.