Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe, Bi. Happiness Seneda, ameongoza sherehe za maadhimisho ya Miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa hotuba yenye kugusia umuhimu wa kuutunza Muungano na kuendeleza umoja wa kitaifa. Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika tarehe 26 Aprili katika Ukumbi wa Mpende Jirani uliopo Vwawa wilayani Mbozi, Bi. Seneda alisisitiza umoja na mshikamano wa Tanzania kama nchi moja, akitoa wito kwa wananchi kuacha mawazo ya kuvunja Muungano.
RAS Seneda, pia aliwahimiza vijana kujikita katika kazi ili kujenga uchumi imara na kufanikisha maendeleo yao binafsi. Alisisitiza kuwa vijana wanaweza kufanikiwa na kujikwamua kiuchumi endapo watajituma na kuwa na malengo thabiti.
Maadhimisho hayo yalihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, wawakilishi wa mashirika ya kiraia, na wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Songwe, waliokusanyika kwa wingi kusherehekea miaka 60 ya Muungano wa Tanzania. Hafla hiyo ilijaa shamrashamra za kipekee, ikionyesha umoja na uzalendo wa Watanzania kuelekea maadhimisho ya kihistoria ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kuunda Tanzania.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.