KITENGO CHA MANUNUZI NA FEDHA MTEGONI UKAMILISHAJI WA MIRADI YA AFYAMBOZI:
Kusuasua kukamilika kwa miradi ya Afya katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi kumewaweka mtegoni watumishi wa Kitengo cha fedha na manunuzi.Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Omary Mgumba amesema ifikapo 30 Juni 2022 kama Kituo cha Afya Hezya, Nambinzo na Halungu vitakuwa havijakamilika watumishi wa kitengo cha Manunuzi na Fedha watapaswa kujitathimini kama wanatosha kwenda na kasi ya Rais Samia Suluh Hassan ndani ya Mbozi na Mkoa wa Songwe.Mkuu wa Mkoa wa Songwe ametoa kauli hiyo wakati akifanya ukaguzi wa miradi ya Afya katika Kituo cha Afya Hezya, Nambinzo na Halungu na kukutana na baadhi ya wajumbe wa Kamati za ujenzi pamoja na wananchi wakilalamika dhidi ya utendaji wa kazi wa Kitengo cha Manunuzi na Fedha kinachopelekea kuchelewa kwa baadhi ya manunuzi."Nimeenda Kituo cha Afya Hezya nimekuta wanalalamikia Kitengo cha manunuzi na fedha na hapa Halungu nao wanalalamikia hivyo hivyo kwa kuchelewesha madokezo" Mhe. Omary Mgumba.Serikali imetoa fedha Milioni 500 ujenzi wa Kituo cha Afya Hezya, milioni 500 ujenzi wa kituo cha Afya Nambinzo milioni 500 fedha za mapato ya ndani ujenzi wa kituo cha Afya Halungu na Milioni 300 Kituo cha Afya Itaka.Elias Mboya mkazi wa Hezya na mjumbe wa Kamati ya manunuzi ameiomba Serikali ipunguze mlolongo wa kwenda na kurudi ili ujenzi ufanyike kwa haraka.Willy Mondya Diwani wa Hezya amesema tatizo lipo upande wa mdokezo kuchelewa kwa mtu kupitia zaidi ya sehemu 3 na ikitokea mtu mmoja hayupo basi dokezo linasimama na kazi zinasimama.Mawazo Tuyanje ameiomba Serikali kuweka utaratibu wa fedha za kuwalipa mafundi zisichukue zaidi ya wiki ili miradi ikamilike na mafundi wafanye kazi kwa bidii.Maarifa Mwashitete ambaye ni Diwani wa Kata ya Halungu ameiomba Serikali kufanya maboresho kwenye. Kitengo cha manunuzi ili wafanye kazi kwa kasi tofauti na sasa.Miradi ya Afya imekuwa inaenda kwa kusuasua licha ya Serikali kuleta fedha za miradi tangu 2021 tofauti na miradi ya Elimu ambayo inakwenda vizuri.MWISHO.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.