• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
SONGWE REGION
SONGWE REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa MKOA WA SONGWE

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Sehemu
      • Mipango na Uratibu
      • Idara ya Elimu
      • Huduma za Maji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Huduma za Serikali za Mitaa
      • Miundombinu
    • Vitengo
      • Huduma za Kisheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
  • Wilaya
    • Mbozi DC
    • Songwe DC
    • Momba DC
    • Ileje DC
  • Halmashauri
    • Mbozi
    • Ileje
    • Momba
    • Songwe
    • Tunduma
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Mifugo
    • Madini
    • Kilimo
    • Biashara
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya na Ustawi Wa Jamii
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma ya Mifugo na Uvuvi
    • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
    • Mipango na Takwimu
    • Ujenzi
  • Machapisho
    • Sheria
    • Miongozo
    • Sera
    • Fomu za Maombi
    • Utaratibu
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MARUFUKU WAGANGA WA JADI KUPOKEA WAGONJWA WASIO NA RIPOTI ZA HOSPITALI

Posted on: April 16th, 2020

Katika jitihada za kupambana na Ugonjwa wa Corona, Chifu wa Mkoa wa Songwe Mbeshena Nzunda ametoa marufuku kwa waganga wa jadi kupokea mgonjwa yeyote ambaye hana ripoti itakayo onyesha tatizo husika limeshindwa kutatuliwa hospitalini.

Chifu Nzunda amebainisha hayo katika kikao cha Kamati ya Amani ya Mkoa ilipokutana kujadiliana hatua zaidi za tahadhari zinazo paswa kuchukuliwa na Mkoa wa Songwe ili kupambana na ugonjwa wa Virusi vya Corona.

Amesema ili mgonjwa apate matibabu kwa mganga wa jadi anapaswa kuonyesha ripoti kuwa baada ya kutibiwa hospitalini hakupona na  wataalamu wa afya wathibitishe hilo pia waganga wa jadi wenye wateja wengi wanapaswa kuwahudumia kwa awamu ili kepusha msongamano.

Chifu Nzunda ameeleza kuwa waganga wa jadi wanatakiwa nao kuchukua tahadhari za Ugonjwa wa Corona kwa kunawa mara kwa mara kwa maji tiririka na sabuni pia kuweka maji hayo kwa ajili ya wateja watakao wahudumia.

Ameogeza kwa kuwataka watumiaji wa pombe za kienyeji kuhakikisha hawachangii vyombo vya kunywea pombe kama ilivyo zoeleka bali kila mmoja awe na chombo chake pia wauzaji  pombe hizo wachukue tahadhari kwa kuweka  maji ya kunawa pia kupunguza misongamano.

Mwenyekiti wa Kamati ya Amani Mkoa wa Songwe Sheikh Hussein Issa amesema kamati hiyo imekubaliana kuchukua baadhi ya hatua ikiwa ni kuongeza tahadhari Zaidi ya Ugonjwa wa Corona huku Uongozi wa Mkoa ukipongezwa kwa jitihada zilizochukuliwa hadi sasa hakuna mgonjwa wa Corona.

Sheikh Issa amesema kuanzia sasa watoto wasiruhusiwe kushiriki katika nyumba zozote za ibada ili kuwaondoa katika hatari ya maambukizi ya Corona pia wazazi wahakikishe watoto wanabaki majumbani.

Ameongeza kuwa nyumba zote za ibada zisiruhusu waumini wengi kujaa bali waingie wachache na wakae mbalimbali bil kusongamana pia maji tiririka ya kunawa na sabuni au vitakasa mikono  viwekwe ndani na nje ya nyumba hizo za Ibada.

Sheikh Issa amesema viongozi wote wa dini mbalimbali wanapaswa kuchukua tahadhari juu ya Ugonjwa wa Corona kwa kufuata maelekezo ya Serikali pia wasiache kumuomba Mungu ili ugonjwa wa Corona usilete maafa katika Nchi ya Tanzania.

 Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. Nicodemus Mwangela ameipongeza kamati hiyo kwa hatua hizo za tahadhari ya Corona huku akimuagiza Mganga Mkuu wa Mkoa wa Songwe kuhakikisha anatoa elimu ya tahadhari ya Corona katika nyumba zote za Ibada.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI January 30, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • SERIKALI YA SAINI MRADI WA ZAIDI YA BILIONI 119.9 UJENZI WA MRADI WA MAJI TUNDUMA VWAWA

    March 20, 2025
  • MKUU WA WILAYA YA ILEJE MHE. FARIDA MGOMI KWA NIABA YA MKUU WA MKOA AFUNGUA HUDUMA YA WIKI YA SHERIA MKOANI SONGWE

    January 25, 2025
  • TASAF MKOA WA SONGWE IMEFANYA ZIARA KUKAGUA MIRADI NA KUJIONEA UTOAJI WA HUDUMA KWA WANUFAIKA WA TASAF MOMBA

    January 03, 2025
  • KIKAO CHA TATHMINI YA HUDUMA ZA AFYA YA UZAZI NA MTOTO MKOANI SONGWE.

    November 07, 2024
  • Angalia zote

Video

ELIMU KWA WATOTO KIPINDI CHA CORONA
Video za Ziada

Kurasa za Karibu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • SALARY SLIP PORTAL
  • AJIRA

Kurasa Mashuhuri

  • IKULU
  • NECTA

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi

    Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE

    Simu: 025 2580305

    Simu ya Kiganjani: 025 2580305

    Barua pepe: ras@songwe.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Sera za Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.