MIRADI YA "FORCE ACCOUNT" YAMFRAHISHA RC MICHAEL, ATOA PONGEZI KITENGO CHA MANUNUZI, FEDHA.
MOMBA: Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Dkt. Francis Michael ameupongeza uongozi wa Wilaya ya Momba pamoja na Halmashauri ya Momba kwa kusimamia vizuri miradi kwa kutumia "Force account"
Mhe. Dkt. Francis Michael amesema hayo baada ya kufanya ukaguzi wa miradi katika Halmashauri ya Wilaya ya Momba na kuona miradi inaendelea vizuri na thamani ya fedha kwenye miradi inaonekana.
Mhe. Dkt. Francis Michael amekagua mradi wa kimkakati wa ujenzi wa machinjio ya kisasa uliopo soko la kisasa la kakozi ambao unathamani ya shilingi Bilioni 2, ukamilishaji wa zahanati ya Nakawale wa kwa thamani ya milioni 50.
Pia, ujenzi wa wa shule mpya ya sekondari ya Ikana ya thamani ya milioni 470, jengo la utawala la Bilioni 2, ukamilishaji wa Nyumba ya Mkurugenzi milioni 150 na ujenzi wa Hospitali ya Wilaya jengo la wodi ya wazazi milioni 500 miradi yote inaendelea vizuri na thamani ya fedha inaonekana.
Nimeona miradi yenu inaendelea vizuri, viwango vizuri, inaonyesha jinsi gani hapa Kitengo cha manunuzi na fedha wanafanya kazi vizuri, miradi inaenda kwa wakati, kwa kweli hongereni sana Momba, amesisitiza Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Dkt. Francis Michael.
Pia, Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Dkt. Francis Michael amesema sehemu nyingi hapa nchini miradi inayotekelezwa kwa "Force account" inakuwa inakwamishwa na watalamu wa Manunuzi na Fedha lakini kwa hapa Momba naona ilo jambo halipo kazi inafanyika vizuri, sijasikia changamoto ya kukwamishwa vifaa, kazi nzuri kwa Mkurugenzi wa Halmashauri na timu yako.
Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi Halmashauri ya Wilaya ya Momba, Bi. Safina Shapwata amesema ushirikiano mkubwa wanaopata kutoka kwa Mkurugenzi wao, Bi. Regina Bieda ndio chachu ya wao kufanya vizuri kwa mambo mbalimbali
Kwa kweli tumefarijika sana Mkuu wa Mkoa kutambua na kuona tunafanya kazi nzuri, nasi tunamhaidi kuwa tutafanya kazi na hatutamuangusha, amesema Bi. Safina Shapwata.
MWISHO.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras.songwe@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.