Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Dkt. Francis K. Michael, amefanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Mji Tunduma. Ziara hiyo ililenga kufuatilia maendeleo ya miradi mbalimbali inayoendelea, na kuhakikisha kuwa miradi hiyo inakamilika kwa wakati na kutoa manufaa kwa wananchi. Baadhi ya miradi iliyokaguliwa ni pamoja na:
|
|||
|
|
|
|
Mradi wa Bwawa la Maji Chiwanda ametembelea eneo la mradi wa Bwawa la Maji Chiwanda wenye Jumla ya thamani zaidi ya Tshs Bilioni 1.3, ambao unatarajiwa kutoa huduma za maji kwa wananchi wa Vijiji Saba (7) vinavyopakana na bwawa hilo. Mradi huu ulianza mwezi Agosti 2023, na inakadiriwa kukamilika mwezi Januari 2024. Bwawa hilo linasimamiwa na Mamlaka ya Bonde la Ziwa Rukwa, na Mhe. Dkt. Francis alisisitiza umuhimu wa kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati ili kuleta tija kwa jamii.
Kituo cha Afya Chapwa amekagua kituo cha afya Chapwa na kutoa maelekezo kuhusu kuimarisha huduma za afya. Alihakikisha vifaa tiba vipo vya kutosha na kuwahimiza watoa huduma kutoa huduma bora kwa wananchi. Pia, alifanya ukaguzi wa ujenzi unaoendelea wa kituo hicho ili kuhakikisha ubora na kufanikisha kukamilika kwa wakati.
Ujenzi wa Madarasa Mapya Shule ya Sekondari Chapwa amekagua ujenzi wa madarasa mapya Unao endelea katika Shule ya Sekondari Chapwa pamoja na kuzungumza na Wanafunzi wakidato cha kwanza katika Shule hiyo. Alitoa maelekezo kwa wasimamizi wa mradi huo kuhakikisha kuwa madarasa hayo yanakamilika kabla ya Januari 2024 ili kuwezesha kupokea wanafunzi wapya wa kidato cha kwanza pamoja na kuwahidi wanafunzi kujengewa Magoli kwajili ya mpila wa miguu (football) na Mpira wa kikapu (Netball).
Shule ya Sekondari Dkt. Samia SH amekagua maendeleo ya ujenzi katika Shule ya Sekondari Dkt. Samia SH. Aliwataka wasimamizi wa mradi kusimamia ujenzi kwa umakini na kuhakikisha madarasa yanakamilika kwa wakati. Aidha, aliahidi kuwapatia wanafunzi vifaa vya michezo kama magoli ya mpira wa miguu na kikapu.
Kituo cha Afya Mwaka Kati Pamoja na ziara hiyo, Mhe. Dkt. Francis amekagua hali ya kituo cha afya Mwaka Kati na kupongeza mradi kwa hatua uliopo.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.