Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mheshimiwa Dkt. Francis Michael ametekeleza agizo la Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa la kuongea na wafanyabiashara wa stendi ya Malori katika mji wa Vwawa Wilayani Mbozi na kufikia muafaka wa ulipaji wa kodi za vibanda.
Dkt Michael, ametekeleza agizo hilo leo Jumatatu Novemba 27, 2023 ambapo amekutana na wafanyabiashara hao katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi.
Akizungumza katika kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Songwe amesema kuwa Serikali ina nia njema ya kuwasaidia wananchi wake hivyo wawe na imani na Serikali yao.
Baada ya kusikiliza hoja za wafanyabiashara hao, kikao hicho kilitoka na maamuzi ya kila mfanyabiashara kulipa Sh20, 000 kwa mwezi kwa kila kibanda.
Dkt Michael ametoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, Abdallah Nandonde kuwa katika bajeti ya 2024/2025 Halmashauri ihakikishe inatenga fedha kwaajili ya ujenzi wa miundombinu ya kisasa katika vibanda hivyo ili kuleta sura nzuri ya mji wa Vwawa.
"Katika bajeti ya mwakani vibomolewe vibanda vijengwe upya na tutaingia mikataba upya, kwasababu saivi ni vurugu hapa kuna watu wanalipa zaidi, na kuna watu wanaoitwa wenye vibanda hawataki tuongeze bei. Sasa ndio maana nasema nanyi mpate kidogo lakini mwakani pale vibanda vitavunjwa tunaingia mkataba upya" amesisitiza
Amesema kuwa zitatangazwa fomu na watu watajaza ili kutuma maombi na watu wote watafanyiwa tathmini na wanaofanya biashara katika maeneo yale watapewa kipao mbele.
"Wale wanaofanya biashara pale watapewa kipaombele, na mhakikishe vibanda hivyo vinakua vikubwa na vyemye ubora" ameagiza
Awali wafanyabiashara hao walikua wakichangia Sh7,000 ambayo ilionekana Halmashauri inapoteza mapato mengi kwa kutoza kiasi ambacho hakiendani na uhalisia wa bei ya vibanda kwa sasa ambapo baadaye Halmashauri ilipendekeaza Sh30,000 kwa kila kibanda
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.