Dkt. Francis amesema kuwa Mkoa wa Songwe unaongoza kwa idadi ya watoto wanaopata mimba za utotoni, jambo ambalo ni kinyume cha sheria. Alisisitiza kuwa mimba za utotoni zinasababisha watoto kuolewa badala ya kusoma na kuchangia katika ujenzi wa taifa. Pia, alibainisha kuwa baadhi ya wazazi na walezi wanahusika kinyemela katika suala hili.
Mkuu wa Mkoa ametoa agizo kwa Afisa Elimu wa Mkoa wa Songwe na wadau wengine, ikiwemo Jeshi la Polisi, kuwatafuta na kuwachukulia hatua wale wote waliohusika na kukatisha masomo ya wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari. Aidha, wametakiwa kutoa taarifa kuhusu hatua zilizochukuliwa katika suala hili
Mkuu wa Mkoa amewataka wadau, ikiwemo Afisa Elimu wa Mkoa, Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Songwe, na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe, kushirikiana katika uchunguzi wa kesi za watoto wanaokatishiwa masomo au wanaoacha masomo kwa sababu ya mimba za mapema. Pia, ametoa muda wa siku tatu kwa taarifa za uchunguzi kutolewa ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa.
Mkuu wa Mkoa amesisitiza umuhimu wa kulinda haki za watoto na kuwasihi wazazi na walezi kuacha tamaduni zisizofaa za kuwaoza watoto kwa ajili ya mali au kuwaweka kwenye uchungaji wa mifugo. Badala yake, amewahimiza kuwapeleka watoto shuleni ili waweze kujenga mustakabali bora.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.