Mkuu wa wilaya ya Ileje Mhe.Farida Mgomi ametekeleza agizo la Mkuu Wa Mkoa wa Songwe Mhe. Dkt.Francis K Michael Kwa kumrejesha shuleni mwanafunzi anayedaiwa kuacha shule na kwenda kufanya kazi za ndani mjini Tunduma.
Mwanafunzi huyo amekabidhiwa shuleni hapo na mkuu wa wilaya Mhe. Farida Mgomi Novemba 20,2023 mbele ya mkuu was mkoa wa Songwe Dkt.Francis Michael ambapo baada ya kukabidhiwa mkuu wa mkoa ametoa maelekezo mapya kwa ofisa elimu mkoa kuhusu wanafunzi wanafunzi wa kike katika mkoa wa Songwe.
Mhe. Mgomi amesema jitihada za kumpata mwanafunzi huyo zimezaa matunda Kwa kumtafuta na kumkuta akiwa Tunduma Kwa mama ake mdogo kutokana na wazazi kukosa fedha ya chakula ambapo kama ofisi ya mkuu wa wilaya itagharamia Kwa lengo la kumsomesha mwanafunzi huyo.
"Kurejea Kwa mwanafunzi huyu ni faraja Kwa uongozi wa wilaya kuhakisha adhima ya kuanzishwa Kwa shule.ya wasichana wilaya ya Ileje kuwakomboa watoto wakike linatimia ikiwepo kuwasaidia wanafunzi ambao wazazi wao watashindwa kuwatolea michango ya chakula," amesema Mhe. Mgomi.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Songwe amepongeza jitihada za mkuu wa wilaya kufanikisha kumrejesha mwanafunzi huyo huku akiwaasa wanafunzi wa shule hiyo kutumia nafasi hiyo kujiendeleza kielimu.
Dkt. Francis, amemwagiza Afisa elimi mkoa wa Songwe kuhakikisha anafanya zoezi la kutembelea shule zote za bweni za wasichana kubaini wanafunzi walioacha shule kwa kukosa fedha ili wawarejeshe kama ilivyofanyika wilaya ya Ileje katika shule ya wasichana Ileje.
Irene Mwazembe mwanafunzi aliyerejeshwa shuleni hapo amemshukuru mkuu wa wilaya Kwa kujitoa kubeba gharama zote zinazohitajika ikiwepo chakula huku akisema wazazi wake kutojiweza ndiko kulimfanya aache shule.
"Nakuahidi mkuu wa wilaya mbele ya mkuu wa mkoa nitahakikisha fadhira Yako nairejesha Kwa maana ya kusoma Kwa bidii mpaka nifike hatua ya juu zaidi na niwasihi wanafunzi wenzangu msikate tamaa kuendelea na masomo hususani katika shule hii ya wasichana," amesema Irene.
MWISHO.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.