MWALIMU APATA ZAWADI YA MILIONI 1, RC MGUMBA ATAKA WENGINE WAJE KUJIFUNZA KAKOMA SEKONDARI.ILEJE:
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Omary Mgumba ametoa wito kwa Taasisi mbalimbali ambazo zinatekeleza miradi waende Sekondari ya Kakoma wajifunze jinsi ya ukamilishaji wamiradi.Mkuu wa Mkoa amesema hayo alipofanya ziara ya ukaguzi wa mradi wa ukamilishaji wa vyumba 3 vya madarasa katika Sekondari ya Kakoma na kukuta wamekamilisha vyumba 3 vya madarasa kwa fedha ya milioni 25 ikiwa ni ziada ya chumba kimoja na chenji ya Milioni 5 imebaki.Aidha, Mkuu wa Mkoa amepongeza Mkuu wa Shule ya Kakoma, Mwl. Àgrey Kahemila na kumpatia zawadi ya Fedha ya shilingi milioni 1 kwa kufanikisha ukamilishaji wa vyumba 3 vya madarasa na kubakiza chenji pamoja na usimamizi mzuri wa ujenzi wa Sekondari ya Chitete ambayo Serikali imeleta fedha milioni 470."Tunamzawadia Mwalimu milioni 1 kwa sababu ametumia milioni 25 kwa ajili ya ukamilishaji wa vyumba 3 vya madarasa, ambavyo Serikali ingetulazimu tulete fedha Milioni 37.5 madarasa yakamilike, lakini yeye amekamilisha madarasa 3 na chenji milioni 5" Mhe. Omary Mgumba.Mkuu wa Mkoa amesema Mkuu wa Shule ya Kakoma amefanya kitu ambacho Shule nyingi zimeshindwa kufanya, hivyo anastahili pongezi.MWISHO.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.