OPARESHENI MAALUMU VITA DHIDI YA MAGENDO YAKAMATA MAGARI 14.TUNDUMA: Magari 14 yamekamatwa yakiwa na bidhaa za magendo ya thamani ya zaidi Milioni 185 katika Oparesheni Maalumu ya kupambana na magendo katika Mpaka wa Tunduma iliyoundwa na Kamati ya ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Songwe.Mkuu wa Mkoa amesema ayo, Mei 5 akiwa Tunduma wakati wa ukaguzi wa oparesheni maalumu ambayo ilianza 13 Aprili 2022 ikishirikisha vyombo vyote vya Usalama na TRA.Mkuu wa Mkoa amesema Kati ya Magari 14 ambayo yamekamatwa moja linatoka ofisi yake na lingine ni gari ambalo limekuwa likitafutwa kwa miaka mingi bila Mafanikio.Mhe. Omary Mgumba amesema bidhaa za magendo zilizokamatwa ni vitenge, pombe kali, vipodozi vikali vilivyozuiliwa kwa mujibu wa sheria zetu, vipo vifaa vya stationery, mayai, vinywaji na bidhaa za kula."Pamoja na bidhaa izo tumefanikiwa kukamata watu 14 madereva wa magari kati yao wawili tunawashikilia bado na wengine wamekimbia na msako unaendelea dhidi waliokimbia kupitia kwa wamiliki wa magari kwani wao ndio waliowaajiri" Mhe. Omary Mgumba.Pia, Mkuu wa Mkoa amesema Serikali chini ya kikosi kazi inaendelea kuwatafuta watu wote walioingiza magendo nchini kwani gari lenyewe haliwezi kuiba au kuingiza magendo bali kuna mtu ambaye anahusika."Kwa sasa mumiliki wa gari atapigwa faini kwa kosa la gari yake kubeba magendo lakini bado atatusaidia kumpata dereva aliyemuajiri ili naye dereva atupatie mtu aliyepakia au aliyekuwa anapeleka mzigo wa magendo ili tuweze kupunguza au kukomesha vitendo vya magendo" Mhe. Omary Mgumba.Aidha, Mkuu wa Mkoa amesema katika oparesheni hii Maalumu Serikali imefanikiwa kukusanya fedha zaidi ya Milioni 45 za adhabu kwa waliokamatwa.Kaimu Meneja wa TRA Mkoa wa Songwe, Dickson Kamala amesema magendo yote yanaanzia nchi ya Zambia na bidhaa inayoongoza kukamatwa ni vitenge, mayai na vipodozi na Serikali inaandaa utaratibu mzuri kuna bidhaa zitauzwa kwa mnada na nyingine zitafanyiwa uharibifu.MWISHO.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.