RAS SENEDA ATAKA WATALAMU WA ARDHI KUONGEZA KASI YA UPIMAJI MKOA
SONGWE: Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe, Bi. Happiness Seneda amewataka watalamu wa Ardhi kuongeza kasi ya kupanga Mkoa vizuri haswa Yale maeneo ambayo yamekuwa na yanakuwa kwa kasi.
Katibu Tawala ametoa wito huo kwenye kikao kazi cha watalamu wa Sekta ya Ardhi Mkoa wa Songwe kilichofanyika Mei 18 na kuwakutanisha watalamu wa Ardhi kutoka Halmashauri za Mkoa wa Songwe pamoja na Wakurugenzi watendaji wa Halmashauri.
"Kuna maeneo tayari wananchi wamejenga na hakujapangwa vizuri ni kazi yetu watalamu kuendelea na mpango wa kurasimisha ili pakae vizuri, haipendezi kwa Mkoa mpya wa Songwe kuwa na sehemu ambazo hazijapangwa vizuri" Bi. Happiness Seneda.
Pia, Katibu Tawala wa Mkoa, Bi. Happiness Seneda amesema Serikali inawategemea sana watalamu wa Ardhi katika kufanikisha kuupanga Mkoa vizuri kuanzia ngazi ya Mkoa hadi kwenye Halmashauri.
Aidha, Bi. Happiness Seneda ametoa wito kwa watalamu wa Ardhi kufanya kazi kwa kushirikiana na kutengeza timu nzuri ya kufanikisha kuupanga Mkoa. vizuri.
Kamishina wa Ardhi Mkoa wa Songwe, Bwn. Erasto Mosha amewataka watalamu wa Ardhi wawe wanatoa taarifa ya kazi mbalimbali wanazozifanya kwa viongozi wao ngazi ya Kata, Halmashauri, ili jamii ijue kuna kazi inafanyika.
Naye, Msajili wa Hati msaidizi, Frida Mwasulama amewaomba watalamu wa Ardhi ngazi ya Halmashauri kujiandaa na mpango wa kutoa Hati ya umiliki wa sehemu ya jengo (Unit titles) ambao utaruhusu mwananchi aweze kutoa umiliki wa sehemu ya jengo lake, mfano, jengo ya gorofa mumiliki anaweza kuuza sehemu ya juu na mtu aliyenunua akapata hati ya umiliki.
MWISHO.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.