Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Omary Mgumba leo Ijumaa 6 Agosti 2021 ameshiriki sala ya Ijumaa katika Msikiti wa Nuru uliopo Mji wa Vwawa.
Katika Hotuba amewafikishia salamu za Rais wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan za kuendelea kufanya kazi pamoja na kutoa wito kwa waislamu kuendelea kuchukua tahadhari ya ugonjwa wa UVIKO-19 kama watalamu wa Afya wanavyoshauri pamoja na kujitokeza kupata chanjo ya UVIKO-19 kwa kuwa Serikali imefanya utafiti na kujiridhisha usalama wa chanjo hiyo.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.