Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Omary Mgumba ametoa wito kwa wadau wa maendeleo Mbozi, Halmashauri na Serikali kuu kuchukua Jitihada za makusudi kukamilisha vyumba vya madarasa 1520 ambavyo wananchi wa Mbozi walijenga kwa nguvu zao wenyewe mwaka 2019.
"Halmashauri pekee itahitaji Bilioni 16 kukamilisha Maboma aya 1520 au kwa bajeti yake itachukua miaka 4 mapato yote yatumike kukamilisha, kitu ambacho kitachukua muda mrefu sana na wananchi hawawezi kuona thamani ya nguvu zao"., Omary Mgumba.
Mkuu wa Mkoa amewapongeza wananchi wa Mbozi na viongozi wa Wilaya kwa kuweza kufanikisha kujenga maboma 1520 ikiwa ni ziada ya mahitaji ya vyumba vya madarasa 1300 kwa sasa, kwa kweli hii ni kazi kubwa sana kwa wananchi na viongozi.
Mkurugenzi wa Mbozi, Hanji Godigodi amesema Halmashauri kwa sasa inanunua bati 2000 kila robo kupitia mapato ya ndani kwa ajili ya ukamilishaji wa Maboma na Serikali kuu kupitia mradi wa EP4R imekuwa ikikamulisha baadhi ya maboma kwenye Shule.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.