RC MGUMBA ATOA WITO WA KUVITENGENEZA VITUO VYA RASILIMALI KILIMO VYA KATA.MBEYA:
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Omary Mgumba ametoa wito kwa Mikoa ya Nyanda za juu kusini kuvikarabati vituo vya rasilimali Kilimo vya Kata ambavyo viko kwenye baadhi ya Kata ili wananchi wapate fursa ya kujifunza Kilimo na ufugaji bora wakiwa kwenye maeneo yaoMkuu wa Mkoa amesema hayo leo Juni 9 kwenye kikao cha Kanda ya Nyanda za juu kusini cha kujadili maandalizi ya maonesho ya nanenane ambayo Kitaifa yatafanyika Mbeya Agosti 2022."Lengo la vituo rasilimali Kilimo ni kumuwezesha mkulima kujifunza kwa vitendo Kilimo bora na ufugaji maana sio wakulima wote wanaweza kwenda kwenye maonyesho ya nanenane lakini uwepo wa vituo hivyo unawasaidia wakulima" Mhe. Omary Mgumba.Mkuu wa Mkoa amesema, Songwe imejipanga vizuri kuelekea maonyesho haya ya Kitaifa ya nanenane na Mkoa unaandaa makala maalumu ya fursa za Kilimo na ufugaji kwa Songwe.Mwaka 2006 Serikali ilianzisha vituo vya rasilimali Kilimo vya Kata kwa malengo ya kuweka mashamba darasa kwa wakulima dhidi ya mazao mbalimbali wanayolima kwenye maeneo yao pamoja na ufugaji na Songwe vipo katika Kata ya Kamsamba, Kanga na Igamba.MWISHO.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.