RC MGUMBA AWAONDOA HOFU WANANCHI WA KITONGOJI CHA NKANKA KUHAMISHWAILEJE: Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Omary Mgumba amesema Serikali haitawaamisha bila kufuata sheria na muongozo wananchi wa kitongoji cha Nkanka kilichopo kata ya Itumba wilaya ya Ileje ambao wameishi kwenye hifadhi ya msitu wa Ileje Renges kwa takribani miaka 30.Mkuu wa Mkoa amesema hayo baada ya wananchi wa kitongoji cha Nkanka kutoa kero yao kwake kuwa wana hofu Serikali kupitia Wakala wa hifadhi ya misitu (TFS) inataka kuwahamisha kwenye kitongoji chao walichoishi takribani miaka 30 kwa madai wanaishi kwenye hifadhi ya msitu wa Ileje Renges.Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Omary Mgumba amesema kwa mujibu wa sheria ya ardhi inataka mtu yeyote akikaa mahali popote zaidi ya miaka 10 bila kubukuziwa na mtu yeyote mahali hapo ni kwake na kama Serikali ikilazimika kuchukua sehemu hiyo lazima itamuamsha kwa kufuata sheria, itawalipa fidia na kuwatafutia sehemu nyingine.“Wananchi wa Nkanka nyie tulieni fanyeni kazi zenu, kwani kitongoji hichi Serikali inakitambua na imekisajili na kama tutakihitaji lazima tutafuata sheria” Mhe. Omary Mgumba.Meneja wa uhifadhi misitu wilaya ya Ileje, Omary Obedy Ally amesema wanapendekeza kitongoji cha Nkanka kiondolewe kwa usalama na utunzaji wa misitu na vyanzo vya maji ambao vimekuwa tegemeo kwa vijiji vya Itumba na vilivyopo jirani kwa kupata maji.“Msitu wa Ileje Renges ulianzishwa 1956 na kuchapishwa kwenye gazeti la Serikali 28 Agosti 1998 kwa Tangazo la Serikali la namba 549 na hdi sasa msitu unazungukwa na vijiji 10 ikiwemo kijiji cha Itumba ambacho kitongoji cha Nkanka kipo ndani msitu” Omary Obedy Ally.Mwaka 1990, kitongoji cha Nkanka kilikuwa na kaya 17, kaya zinaongezeka siku hadi siku na 2019 kaya zimefika 105 ambazo zinakadiriwa kuwa na wastani ya wananchi 406, Mhifadhi msitu amesema, Omary Obedy Ally.Diwani wa Kata ya Itumba, Mhe. Mohamed Mwala amesema kitongoji cha Nkanka kimesajiliwa na Serikali na wananchi wameshiriki uchaguzi na wamempata Mwenyekiti wa kitongoji, kijiji na Diwanini vyema kama Serikali watakuwa wanahitaji kwa matumizi yao basi wananchi wahamishwe kwa kufuata taratibu na sheria.Mkuu wa wilaya ya Ileje, Mhe. Anna Gidarya amesema kamati ya ulinzi na usalama iliwatafutia viwanja wakazi wote wa Nkanka ili wahame na kupisha eneo la msitu lakini hadi leo hakuna mwananchi aliyeweza kuhama, ndio maana tumeona Mkuu wa Mkoa uje na uongee na wananchi wa Nkanka.Eda Mbughi, mkazi wa kitongoji cha Nkanka amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kuwaondoa hofu juu ya kuhamishwa kwani kwa muda mrefu wamekuwa wakiambiwa wahame na kuwafanya washindwe kujiletea maendeleo kwenye kitongoji chao.Mwenyekiti wa Kitongoji cha Nkanka, Bakari Sikaumba amesema wananchi wa Nkanka wanajitahidi kutunza mazingira na uharibifu unaofanywa na wananchi wanaotoka nje ya kitongoji hicho amewaomba watalamu wa TFS na Halmashauri kushirikiana nao kwa pamoja ili kuweza kuweka mipaka vizuri ikiwa na pamoja na utunzaji wa mazingira.Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Omary Mgumba awetaka wananchi wa ktongoji cha Nkanka kutunza mazingira na wale wote ambao wamelima kwenye vyanzo vya maji basi waondoke haraka kabla sheria haijachukua mkondo wake.Wakati huo huo, Mkuu wa Mkoa amewaagiza TFS na Halmashauri ya wilaya ya Ileje kuanza kuwatambua wakazi wote wa kitongoji cha Nkanka na mali zao pamoja na kuweka mipaka vizuri ili wananchi wasizidi kusogea kwenye hifadhi ya msitu.MWISHO.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.