Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. Nicodemus Mwangela ametoa siku 14 kwa kampuni Tanzu ya TANESCO, ETDCO kukamilisha ujenzi wa laini kuu ya umeme Mkoani hapa.
Brig. Jen. Mwangela ametoa agizo hilo wakati akifanya ziara ya ukaguzi wa laini kuu ya umeme inayojengwa kutoka Kituo cha Umeme Iyunga Mkoa wa Mbeya hadi Selewa Mbozi katika kituo cha kutawanyia umeme kwa Mkoa wa Songwe.
Ujenzi wa laini hiyo ulitakiwa kukamilika Machi 31 kwa kumjibu wa mkataba ili kuondoa kero ya umeme kukatika mara kwa mara Mkoani Songwe.
"Nimeongea na Meneja wa ETDCO na kumueleza juu ya umuhimu wa kukamilika haraka kwa mradi huu ndani ya siku 14 na ameniahidi atafanya hivyo.”, Brig. Jen. Mwangela.
Aidha ameagiza kuongezwa kwa wafanyakazi ili mradi ukamilike ndani ya siku 14 licha ya kuwa hadi sasa baadhi ya mafundi wanaendelea na kufunga nyaya kwenye laini kuu na wamefika eneo la Nanyala wakitokea Mbozi.
Ziara ya Mkuu wa Mkoa inafanyika ikiwa ni kufuatilia utekelezaji wa mradi huo ambapo Mkuu wa Mkoa aliambatana na Kamati yake ya Ulinzi na Usalama.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.