SONGWE: RC MWANGELA AWATAKA WAFANYABIASHARA KUUZA BIDHAA KWA BEI ELEKEZI
Wafanyabiashara wa Mkoa wa Songwe wametakiwa kuuza bidhaa zao kwa kuzingatia bei elekezi iliyopo na si kuongeza bei bila sababu za msingi.
Agizo ilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Breg. Jen. Nicodemus Mwangela alipokutana na wafanyabiashara kwenye kikao kazi, 28 Novemba 2020.
“Kuongeza bei za bidhaa kwa makusudi wakati hazijapanda uko ni kumchonganisha mwananchi na Serikali yake kitu ambacho hatutakubali” Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Mwangela.
Miezi ya hivi karibuni kumekuwa na ongezeko la bei ya saruji na baadhi ya bidhaa wakati Serikali haijaongeza tozo ya aina yeyote na malighafi ya kutengeneza bidhaa zipo hapa hapa Tanzania.
Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa amewaomba wafanyabiashara wa Songwe kuwekeza katika viwanda vya mnyororo wa thamani wa mazao yanayozalishwa kutokana na Mkoa kuwa na maligahfi za kutosheleza viwanda hivyo pamoja na kuwekeza katika ujenzi wa Hoteli.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.