RC MWANGELA: WANANCHI WAPEWE ELIMU ZAIDI KUONGEZA HIFADHI YA KIMONDO
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Breg. Jen. Nicodemus Mwangela amewaagiza viongozi wa Wilaya ya Mbozi kuendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya faida ya kuongeza ukubwa wa eneo la hifadhi ya Kimondo lililopo kijiji cha ndolezi Kata ya Mlangali ambalo kwa sasa liko chini ya Mamlaka ya uhifadhi wa Ngorongoro.
Mkuu wa Mkoa ametoa agizo ilo alipokutana na Serikali ya Kijiji cha Ndolezi kufuatia baadhi ya wananchi kutoelewa vizuri mchakato wa fidia na faida ya kuongeza ukubwa wa eneo la Kimondo ambalo kwa sasa liko chini ya Mamlaka ya uhifadhi wa Ngorongoro.
Serikali kupitia Mamlaka ya uhifadhi wa Ngorongoro ina mpango wa kuchukua Ardhi kwa fidia kwa baadhi ya wananchi wanaozunguka eneo la Kimondo kwa ajili ya kuleta wanyama mbalimbali pamoja na kuboresha miundombinu na kukifanya Kimondo cha Mbozi kuwa eneo la utalii kwa Mkoa wa Songwe.
Mkuu wa Mkoa amesema jambo ili ni la hiari linaitaji elimu zaidi na wananchi wakikubaliana kwa hiari basi serikali itakuja kufanya tathimini kwa kina na kila mtu atalipwa fidia yake kwa mujibu wa sharia na taratibu ndani ya miezi sita baada ya Serikali kufanya tathimini.
Pia, Mhe. Mwangela ametoa wito kwa wananchi ambao hawakubaliani na swala ili kwa sababu za kutokuwa na uelewa juu ya swala ili kutowatishia maisha au kuwaogopesha wale ambao wamekubali Ardhi yao ichukuliwe kwani jambo ili Serikali italifanya baada ya wananchi wote kukubaliana juu ya ili.
Bi. Celina Mwanda mkazi wa Ndolezi ambaye Ardhi iko eneo ambalo linahitajika na Ngorongoro ameiomba Serikali kuendelea kutoa elimu ya jinsi fidia itakavyolipwa kwenye mashamba pamoja na makazi ndio sababu kubwa ya baadhi ya wananchi wameshindwa kulipokea vizuri.
Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Mhe. John Palingo amesema wamefanya mikutano na Serikali ya Kijiji pamoja na wananchi na kuwaeleza juu ya kuchukua ardhi yao kwa fidia kwa ajili kuongeza eneo la Kimondo na kuna baadhi ya wananchi wamekubali na kulipokea na wengine bado wamegoma kwa kuwa bado hawajaelewa vizuri.
Mbunge wa Jimbo la Vwawa, Mhe. Japhet Hasunga amesema kimondo hiki ni cha miaka mingi lakini hakikuwa na thamani lakini baada ya mimi kuteuliwa na Rais kwa nafasi ya Naibu waziri wa Utalii Serikali ilianza mchakato wa kukitangaza Kimondo cha Mbozi kwa kuleta pesa ya kujenga jengo la kisasa pamoja na kuanzisha siku ya Kimondo Duniani ambayo hufanyika mwishoni mwa mwezi Juni kila mwaka.
“Tusiwaze sana Kilimo sehemu ambazo kuna shughuli za utalii wananchi wanatengeneza pesa nzuri kuliko sisi tunaofanya Kilimo jambo ili la utalii liko vizuri tunachotaka ni taratibu za fidia zifuatwe” Mbunge wa Jimbo la Vwawa, Mhe. Japhet Hasunga.
Mhe. Hasunga amesema eneo ili Ngorongoro wakileta wanyama pamoja na kuliboresha vizuri litakuwa eneo nzuri kwa ajili ya kufanya utalii kwa Mkoa wa Songwe na vijana wa kijiji cha ndolezi watapata ajila na kuboresha maisha yao.
Serikali ya Mkoa wa Songwe kwa kushirikiana na Mamlaka ya Uhifadhi wa Ngorongoro wanampango wa kukifanya Kimondo cha Mbozi na eneo ilo kuwa na vivutio mbalimbali vya utalii.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.