"Mkoa wa Songwe umekuwa ukifanya vizuri kwenye Kilimo hadi kushika nafasi 3 kitaifa, kutokana na fursa ya soko la mafuta ya kula hapa Tanzania ni vyema wakulima waanze kulima zao la Alzeti kwani soko lake lipo na uhakika" Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Omary Mgumba.
"Kwani kama Nchi tunaagiza takribani Tani 500,000 za mafuta ya kula wakati fursa ya kuzalisha tunayo na malighafi tunazo ambazo ni zao la Alzeti ambalo kwa Songwe linakubali vizuri" Mhe. Omary Mgumba.
"Ni wakati sasa kama Mkoa kuja na mkakati wa viwanda vidogovidogo vya kuzalisha mafuta ya kula ambayo yatatokana na Alzeti" Mhe. Omary Mgumba.
"Ni wakati sasa wakulima wetu walime kutokana na mahitaji ya soko ya mazao sokoni kama Alzeti na mazao mengine ili kukabiliana na upungufu wa mafuta hapa Nchini" Mhe. Omary Mgumba.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.