SENSA KWENDA KUFANIKISHA ZOEZI UVISHAJI WA HERENI ZA MIFUGO.
Na. Nicholas Ndabila
SONGWE: Ifikapo tarehe 23 Agosti 2022 Nchi itafanya zoezi la Sensa ya watu na makazi, ambapo moja ya taarifa zitakazokusanywa ni pamoja na idadi ya mifugo iliyopo katika Kaya na aina ya ufugaji unaotumika.
Afisa Mifugo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Omary Kapeyu amesema baada ya zoezi la Sensa litakalo saidia kutoa takwimu sahihi za idadi ya mifugo na sehemu inakopatikana itawasaidia watalamu Kuongeza nguvu ya kutoa elimu kwa wafugaji juu ya umuhimu wa mifugo kutambuliwa kwa kuvalishwa heleni za kielotriniki tofauti na sasa ambapo zoezi linaenda kwa kazi ndogo.
Afisa Mifugo ametoa wito kwa Wafugaji wote kujitokeza kwa wingi kuhesabiwa na kuwapa ushirikiano makalani wa Sensa watakapopita katika maeneo yao, Aidha, wafugaji wanashauriwa kutoa takwimu sahihi wakati wa zoezi hilo ili kuiwezesha Serikali kupanga mipango ya Maendeleo.
Mkoa wa Songwe ulipokea hereni elfu 68,100 kwa ajili ya Ngombe, Mbuzi, Punda na Kondoo hadi sasa ni mifugo elfu 1760 tayari imeshatambuliwa kwa kuvalishwa hereni na zoezi bado linaendelea.
Aidha, Afisa Mifugo Mkoa wa Songwe, Ndg. Omary Kapeyu ameeleza Faida za Mifugo kuwa na hereni ya kielektroniki ni kuwa mifugo itatambulika mahali ilipo na umiliki wake, Kukabiliana na magonjwa ya mlipuko, Kuwa na hakikisho la usalama wa chakula, Kurahisisha biashara ya Mifugo na mazao yake ndani na nje ya nchi, Udhibiti wa wizi wa mifugo, Kurahisisha upatikanaji wa mifugo iliyopotea, Kurahisisha uboreshaji wa koosafu za mifugo na mwisho kabisa Utambuzi utawezesha urahisi wa upatikanaji wa mikopo na bima ya Mifugo.
“kwa sasa ifikapo Septemba 2022, mfugo ambayo itakuwa haijavalishwa heleni haitaruhusiwa kuingia machinjioni kuchinjwa, Haitaruhusiwa kuuzwa katika Minada, Haitaruhusiwa kutumika kutolewa mahari, hivyo nitoe wito kwa wafugaji kuchangamkia kuweka heleni za kieletroniki kupunguza kadhia zitakazojitokeza” Ndg. Omary Kapeyu Afisa Mifugo Mkoa wa Songwe.
Bei elekezi ya kuvisha heleni za kielotriniki kwa Mifugo ni shilingi 1,750 Ng'ombe na Punda huku Mbuzi na Kondoo ikiwa ni shilingi 1,000 na changamoto kubwa ya zoezi ili ni wafugaji wa kuhama hama.
MWISHO.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.