SERIKALI YAAGIZA KITUO CHA AFYA NDOLA KUANZA KAZI
ILEJE: Serikali ya Mkoa wa Songwe imeagiza Kituo cha Afya Ndola kianze kutoa huduma kuanzia tarehe 29 Agosti 2022 kwa huduma za wagonjwa wa nje na maabara.
Agizo ilo limetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Mhe. Cosmas Nshenye ambaye ni muwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Songwe wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi wilayani Ileje, 25 Agosti 2022.
Muwakilishi wa Mkuu wa Mkoa ametoa agizo ilo kufuatia kukamilika kwa jengo la wagonjwa wa nje na maabara baada ya Serikali kuleta fedha za awali milioni 250 fedha za tozo za miamala kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Afya Ndola.
Katibu Tawala Mkoa wa Songwe, Bi. Happiness Seneda amesema majengo yamekamilika tayari hakuna sababu ya kuendelea kusubiria hadi yakamilike mengine wakati huduma zinaweza kuanza kwa majengo yaliyopo kama la wagonjwa wa nje na maabara.
"Mkurugenzi simamia ili leta watumishi na vifaa tiba pamoja na dawa, wananchi waanze kupata huduma hapa uku wakisubiria kukamilika kwa majengo mengine" Bi. Happiness Seneda.
Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Mhe. Anna Gidarya amesema tayari Serikali kuu imeleta fedha milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Afya Ndola, fedha ambazo zinatokana na tozo za miamala.
MWISHO.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.