SILINDE: KITONGOJI CHA NKANKA KUPATA SHULE, BARABARA.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. David Silinde amesema baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuridhia wananchi wapatao 3,000 wanaoishi katika hifadhi ya msitu wa Ileje Renger katika kitongoji cha Nkanka Kijiji cha Itumba wilayani Ileje kuendelea kubaki Serikali itaanza ujenzi wa shule shikizi ya msingi na barabara.
Mhe. David Silinde ameyasema hayo leo Oktoba 25, 2022 katika ziara ya kamati ya mawaziri wa kisekta inayoshughulikia migogoro ya Ardhi ilipokuwa inaongea wananchi wa kitongoji cha Nkanka, ambao kitongoji hicho kipo katikati ya hifadhi ya msitu wa Ileje Renger na ambao wameishi hapo kwa zaidi ya miaka 40.
Mhe. Silinde amesema baada ya mchakato wote kukamikika, ujenzi wa shule ya msingi shikizi utaanza na badae itasajiliwa kuwa shule kamili kwa kuwa ni dhamira ya mheshimiwa Rais kumaliza changamoto zote za miundombinu kwenye sekta ya elimu.
Mhe. Silinde amesema ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kuwa ifikapo 2027 changamoto za miundombinu kwenye elimu nchini ziwe zimemalizika kabisa na analeta fedha nyingi za kumaliza changamoto za miundombinu kwenye elimu.
Mhe. David Silinde amesema Ofisi ya Rais-TAMISEMI inasimamie miradi nmikubwa ya kutatua changamoto za miundombinu katika elimu hapa nchini, ukiwemo mradi Boost una fedha zaidi ya tirioni 1.1 ambazo kazi yake ni nikuboresha elimu ya msingi kwa kujenga shule mpya na kuboresha zilizopo, mradi wa SEQUIP kwa ajili ya kujenga Sekondari mpya kwenye kata ambazo hazina, mradi wa lipa kulingana na matokeo (EP4R)
Kuhusu Barabara ya Nkanka, Mhe. Silinde amesema baada kumaliza changamoto TARURA Ileje watakuja kuisajili ili Serikali itoe fedha na iweze kutengenezwa vizuri.
Agnes Nyondo mwananchi wa kitongoji cha Nkanka amesema baadhi ya viongozi kuwaambia wahame wamejikuta wanashindwa kufanya mambo ya maendeleo, kama kujenga ,na kulima kwani wamekuwa wakiishi kwa hofu, hivyo wamemshukuru Rais Samia kwa uhamuzi wake wa kuwataka wabaki katika eneo hilo
MWISHO
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.