Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Omary Mgumba amesema Mkoa umejipanga kuamasisha wakulima kulima mazao ya mafuta ili kukabiliana na uagizaji wa mafuta Nje ya Nchi unaopelekea mafuta kuadimika na bei kuwa juu, mazao ambayo yanalengwa ni Alzeti, Karanga, Soya na Michikichi.
Mhe. Omary Mgumba ameongea ayo wakati wa makabiziano ya miche ya michikichi 20,000 kwa Mkoa wa Mbeya na Songwe kutoka ASA, hafla iliyofanyika Magamba Mbozi.
Mhe. Mgumba amekabidhi Miche 20,000 kwa Mkoa wa Songwe na Mbeya, kwa Songwe Wilaya ya Songwe na Momba zimepata miche 2,500 kila moja na Busukelo na Kyela zimepata 7,500.
"Serikali kukabiliana na tatizo la upungufu wa mafuta ya kula imeanza kutoa bure miche ya michikichi ili wakulima walime sehemu inayokubali na hapa Songwe kuna maeneo ya Momba na Mbozi inakubali awali miche hii iliuzwa kati ya 2,000 hadi 3,000 lakini Serikali imeamua kugawa bure kwa wananchi ili kukabiliana na upungufu wa mafuta ya kula"
Omary Mgumba.Pia, Mkuu wa Mkoa ametoa wito kwa wakulima kuongeza uzalishaji wa Alzeti kwa kuwa mafuta yatokanayo na Alzeti mkulima mwenyewe anaweza kujikamulia na kuondokana na upungufu lakini kutokana na viwanda vinavyojengwa Songwe vitahitaji sana Alzeti hivyo ni fursa kwa wakulima kuzalisha Alzeti na mazao mengine kama Soya na Karanga ya kutosha.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.