• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
SONGWE REGION
SONGWE REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa MKOA WA SONGWE

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Sehemu
      • Mipango na Uratibu
      • Idara ya Elimu
      • Huduma za Maji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Huduma za Serikali za Mitaa
      • Miundombinu
    • Vitengo
      • Huduma za Kisheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
  • Wilaya
    • Mbozi DC
    • Songwe DC
    • Momba DC
    • Ileje DC
  • Halmashauri
    • Mbozi
    • Ileje
    • Momba
    • Songwe
    • Tunduma
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Mifugo
    • Madini
    • Kilimo
    • Biashara
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya na Ustawi Wa Jamii
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma ya Mifugo na Uvuvi
    • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
    • Mipango na Takwimu
    • Ujenzi
  • Machapisho
    • Sheria
    • Miongozo
    • Sera
    • Fomu za Maombi
    • Utaratibu
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

SONGWE KUJIFUNZA USAFI WA MAZINGIRA NJOMBE

Posted on: April 19th, 2021

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. Nicodemus Mwangela leo ameongoza viongozi na wataalamu wa Afya Mkoa wa Songwe kufanya ziara ya kujifunza utekelezaji wa kampenzi ya usafi wa mazingira kwa Mkoa wa Njombe ambao unafanya vizuri kwa sasa kitaifa.

Brig. Jen. Mwangela amesema lengo la ziara hiyo ni kujifunza ili kuongeza ujuzi na maarifa yatayowezesha Mkoa wa Songwe kufanya vizuri zaidi katika utekelezaji wa kampeni hiyo kwakuwa sasa bado mkoa huo haufanyi vizuri.

“Nawapongeza sana Mkoa wa Njombe kwa kufanikisha kufanya vizuri katika usafi wa mazingira, sisi tupo tayari kujifunza ndio mana nimekuja na timu kubwa ya viongozi wote, tunataka kuijua siri ya mafanikio yenu.”, amesema Brig. Jen. Mwangela.

 Katibu Tawala Mkoa wa Songwe Dkt Seif Shekalaghe amesema ziara hii itasaidia pia kujitathimini endapo suala la usafi wa mazingira ni ajenda inayoshikiliwa na viongozi wa ngazi zote kuanzia ngazi ya vijiji hadi wilaya kwani tangu tumepata uhuru zaidi ya miaka hamsini suala la usafi wa mazingira bado ni tatizo.

Dkt Shekalaghe amesema kila kiongozi anapaswa kujiuliza endapo anaitendea haki nafasi yake na kama kungekuwa na ushirikiano na kujitoa kwa viongozi wa ngazi zote tatizo hilo lingekua limeisha.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Songwe Dkt Hamad Nyembea amesema Mkoa wa Songwe haufanyi vizuri katika usafi wa mazingira licha ya kwamba hautofatiani na mikoa mingine kwa maana ya wataalamu wa afya na fedha zinazotolewa na serikali.

Dkt Nyembea amesema ziara hiyo itasaidia wataalamu wa Afya kujua na kushuhudia kwa kujionea wenyewe mbinu walizotumia wenzao wa Mkoa wa Njombe wakafanikiwa katika usafi wa mazingira.

Kwa Upande wake Mkuu wa Mkoa wa Njombe Marwa Mwita Rubirya amesema mkoa huo ulianza kutekeleza kampeni ya usafi wa mazingira mwaka 2012 wakati Mkoa huo una anzishwa na kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kama UNICEF wamefanikiwa kufanya vizuri kitaifa na kupata zawadi ya magari, pikipiki na fedha.

Rubirya amesema katika kutekeleza kampeni hiyo wamehakikisha wananchi na taasisi zote wanajenga vyoo na kuvitumia, jamii ilihamasishwa kuweka mazingira safi na kuzingatia kanuni bora za afya na kubadili tabia ya kuishi kwa mazoea mabaya ya uchafu.

Amesema kutokana na jitihada walizoweka hadi kufikia Disemba 2020 asilimia  77 ya kaya zote Mkoani Njombe zina vyoo bora, huku asilimia 68 ya kaya zina vyoo na vifaa vya kunawia, asilimia 42 ya shule za msingi na sekondari zina vyoo bora huku vituo vyote vya kutolea huduma za afya vikiwa na vyoo bora.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI January 30, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • SERIKALI YA SAINI MRADI WA ZAIDI YA BILIONI 119.9 UJENZI WA MRADI WA MAJI TUNDUMA VWAWA

    March 20, 2025
  • MKUU WA WILAYA YA ILEJE MHE. FARIDA MGOMI KWA NIABA YA MKUU WA MKOA AFUNGUA HUDUMA YA WIKI YA SHERIA MKOANI SONGWE

    January 25, 2025
  • TASAF MKOA WA SONGWE IMEFANYA ZIARA KUKAGUA MIRADI NA KUJIONEA UTOAJI WA HUDUMA KWA WANUFAIKA WA TASAF MOMBA

    January 03, 2025
  • KIKAO CHA TATHMINI YA HUDUMA ZA AFYA YA UZAZI NA MTOTO MKOANI SONGWE.

    November 07, 2024
  • Angalia zote

Video

ELIMU KWA WATOTO KIPINDI CHA CORONA
Video za Ziada

Kurasa za Karibu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • SALARY SLIP PORTAL
  • AJIRA

Kurasa Mashuhuri

  • IKULU
  • NECTA

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi

    Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE

    Simu: 025 2580305

    Simu ya Kiganjani: 025 2580305

    Barua pepe: ras@songwe.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Sera za Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.