SONGWE: WANANCHI WAHIMIZWA KUPIMA UKIMWI KUJUA HALI ZAO KUEPUKA MAAMBUKIZI MAPYA
Wananchi wa Mkoa wa Songwe wahimizwa kupima UKIMWI kujua hali zao za maambukizi hii inatokana na Mkoa kuwa na 86% ya watu wanaoishi na UKIMWI kufahamu hali zao wakati lengo la kitaifa tunatakiwa kufika 90% au zaidi watu kujua hali zao za maambukizi kwa wanaoishi na UKIMWI.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Breg. Jen. Nicodemus Mwangela amewataka watalamu wa Afya ifikapo Desemba 2021 kuhakikisha Mkoa uwe umetimiza lengo la 90% kwa kuwafikia wananchi wote ambao wanapaswa kujua hali zao za maambukizi ya UKIMWI.
Mkuu wa Mkoa ametoa agizo ilo katika maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani ambayo ufanyika kila Desemba mosi nas kwa Mkoa yamefanyika Wilaya ya Mbozi eneo la Ivungwa-Karasha na Hotuba ya Mkuu wa Mkoa kusomwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Mhe. John Palingo.
“Kwa kutofanya vizuri katika 90 ya kwanza kutapelekea watu wanaoishi na UKIMWI kutotambua hali zao hali ambayo itapelekea kuongezeka kwa maambukizi mapya katika jamii na kupunguza kasi ya kupambana na UKIMWI, kwani msimamo wa Mkoa wa Songwe ni kuwa Mkoa wa kwanza ifikapo 2030 kwa kumaliza kabisa maambukizi mapya ya UKIMWI, vifo vitokanavyo na UKIMWI na kutokomeza ubaguzi kwa walioathirika na UKIMWI huu utakuwa mchango wetu mkubwa kwa Tanzania” Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Breg. Jen. Nicodemus Mwangela.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Dr. Hemed Nyembea amesema mikakati ya 90 tatu za kupambana na UKIMWI Songwe tunafanya vizuri kwenye 90 ya pili na tatu tub ado nguvu inatakiwa katika 90 ya kwanza, 90 ya kwanza watu wote wanaoishi na UKIMWI waweze kupima na kutambua hali zao, 90 ya pili wote waliopata UKIMWI kuanzishiwa dawa za kufubaza kwa 90 ya pili tumefika 96% na kwa 90 ya tatu inataka wote wanaoishi na UKIWMI wanaendelea kupata Dawa Songwe tumefika 95%.
Dr. Nyembea amesema Mkoa unaendelea na mkakati wa kupamba na UKIMWI kwa kuendelea kutoa ya huduma ya kupima kwa wananchi kwa kulengwa wale wenye sifa, kujikita kubaini watu wote wenye sifa ya kupimwa UKIMWI wanapokuja kwenye vituo vya kutolea Huduma pamoja na kuendeleza mkakati wa kufika lengo la 90 ya kwanza.
Mkazi wa Mbozi, Eliud Mwashambwa ameiomba Serikali kuendelea kuhamasisha watu wapime UKIMWI kupitia mikusanyiko mbalimbali inayokuwepo ili kuweza kutimiza lengo la 90% ya watu wanaoishi na UKIMWI kutambua hali zao.
Dr. Antony Galishi kutoka Worldvision Tanzania amesema shirika linaendelea kutoa elimu juu ya ukatili ya kijinsia na watoto katika makundi mbalimbali kwa kuwa ukatili nao umekuwa ni moja ya chanzo cha maambukizi mapya ya UKIMWI na lengo ni kuhakikisha ifikapo 2030 hakuna maambukizi mapya.
Mkoa wa Songwe una vituo vya Tiba ya Matunzo (CTC) 64 na vituo vya kukinga maabukizi ya UKIMWI kutoka kwa Mama kwenda kwa Mtoto 108.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.