TANROADS KWA KUSHIRIKIANA NA WADAU KUURUDISHA MTO ZIRA KWENYE NJIA KUU, ENEO LA MBALA KANGA LIPITIKE MUD WOTE.
SONGWE: Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenya ameiagiza Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kushirikiana na Mamlaka ya Bonde la Ziwa Rukwa kumaliza tatizo la kufurika na kuhama mto zira na kusababisha mawasiliano kati ya mji wa Mbalizi na Mkwajuni wilayani Songwe kukatika.
Kasekenya alitoa kauli hiyo wakati alipotembelea eneo hilo ambalo limekuwa linafurika Maji wakati wa masika na kusababisha mawasiliano kukatika ambapo Naibu Waziri huyo alisema ili kumaliza tatizo la mto huo kuhamahama ni lazima mamlaka ya Bonde la ziwa Rukwa ishiriki ili kuweza kutoa mwongozo utakaosaidia kumaliza tatizo linalojitokeza Mara kwa Mara.
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhe. Mhandisi, Msongwe Kasekenya (MB) amefanya ziara ya kutembelea Barabara ya Mbalizi-Mkwajuni katika eneo la Mbala-Kanga ambapo TANROADS Songwe wanajenga Box karavati 7 kwenye tuta la Barabara pamoja na kufika hadi eneo ambalo Mto Zira umeanza kuchepuka na kuacha Njia Kuu umbali wa kilometa 3.5 kutoka kwenye Daraja la Mto Ziara.
" Tutashirikiana na Bonde la Ziwa Rukwa ili waweze kutupa muongozo mzuri kwa sababu wao ndio wanahusika na maswala ya mito na maziwa lakini TANROADS itatoa utalamu wa namna ya kutengeneza Kingo" alisema na kuongeza.
"Kwa hali ilivyo hapa Mto Ziara ni lazima tutafute fedha kwa njia yeyote kwa kushirikiana na wadau wengine kama Mazingira, Wizara ya Mifugo, TAMISEMI ili tuweze kidhibiti hali hii" alisema Kasekenya.
Meneja wa TANROADS Mkoa wa Songwe, Mhandisi Yohana Kasaini alisema kutokana na mafuriko yaliyotokea Serikali ilitoa Milioni 727 kwa ajili ya kujenga Box karavati 4 katika eneo la tuta la Barabara la Kanga-Mbala ambayo ni madaraja ya kudumu kwa ajili ya kuvusha maji ili lisiweze kubomolewa, lakini TANROADS Songwe imeweza kuongeza Box karavati 3 jumla kutakuwa na Box karavati 7 eneo la tuta la Barai la Kanga-Zira.
Mhandisi Kasaini alisema kwa ukarabati uliofanyika katika tuta la Kanga-Zira watakuwa wamefanikiwa maji yaweze kupita lakini ili kufanikiwa kwa 100% inatakiwa kazi ya kurudisha njia Kuu ya Mto Zira ifanyike kwa haraka ili maji yapite kwenye njia yake na TANROADS Songwe ifikapo mwishoni mwa Octoba tutakuwa tumemaliza ujenzi wa boxi karavati 7 kabla ya Mvua haijaanza.
Mbunge wa Jimbo la Songwe, Mhe. Philip Mulugo amesema wananchi kutoka katika Kata 8 wamekuwa wakiathirika kukatika kwa mawasiliano kipindi cha Mvua katika eneo la Kanga-Zira na kusababisha kuwaongezea gharama ya maisha kwani iliwarazimu kuzunguka hadi Mkoa wa Mbeya ili waweze kufika makao makuu ya Wilaya ya Songwe.
Aidha, Mulugo amemuomba Waziri Barabara ya Mbalizi-Mkwajuni hadi Patamela ichukuliwe kwa umhimu wake iweze kujengwa kwa kiwango cha lami ndani ya muda mfupi na amemuomba kufikisha kilio cha wana Songwe kwa Rais wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya kuwasaidia.
Mkuu wa Wilaya ya Songwe, Simon Simalenga amesema Songwe ni Wilaya ya kimkakati kiuchumi kwa Nyanda za Juu Kusini kutokaa na madini yanayochimbwa sasa, lakini sasa kuna madini ya Rare Earth yataanza kuchimbwa Songwe, madini ambayo Duniani yanapatikana Nchi ya China na Tanzania tu, hivyo amemuomba Waziri kuweza kuitazama Barabara ya Mbalizi-Mkwajuni hadi Patamela kwa umhimu wake amewaomba viongozi wakuu wa Nchi, Waziri Mkuu, Makamu wa Rais na Rais waweze kuwasaidia kupata Barabara ya Lami kwa sababu ya fursa za kiuchumi zilizopo Songwe za manufaa ya Mkoa na Taifa.
Aidha, Mkuu wa Wilaya amesema ofisi yake kwa kushirikiana na Mbunge wa Songwe, TANRROADS Songwe na wadau wote waliopo Songwe watashirikiana kuhakikisha wanahakikisha Mto Zira unarejea kwenye njia yake Kuu na lengo lake ni kuhakikisha ndani ya miezi 2 Mto Zira unarudi kwenye Njia Kuu yake.
Kwa kipindi cha miaka 2 mfululizo mawasiliano ya Barabara ya Mbalizi-Mkwajuni kukatika katika eneo Kanga na Zira, juhudi mbalimbali za Viongozi wa Mkoa kwa kushirikiana na Mgodi wa SHANTA pamoja na TANROADS za kujaza kifusi kwenye tuta la Kanga na Zira na kutumia makontena zimekuwa na mbinu za muda mfupi na kufanya hali kujiridia mara kwa mara, lakini juhudi zinazofanywa sasa na TANROADS za kujenga boksi karavati 7 na Mpango wa kurudisha njia Kuu ya Mto Zira zinaonyesha zinaweza kuwa njia ya kudumu kwa watumiaji wa Barabara ya Mbalizi-Mkwajuni.
Mwisho.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.