TIMU YA WATALAMU WA AFYA YAANZA KUFUATILIA SABABU YA VIFO VYA UZAZI KWENYE JAMII.
SONGWE: Katika kuhakikisha vifo vya uzazi vinapungua au kumalizika kabisa Timu ya Afya Mkoa wa Songwe (RHMT) kwa kushirikiana na Timu za Afya za Halmashauri (CHMT) wameanza kufuatilia kwenye jamii ambapo kifo cha mzazi kimetokea kwa kushirikiana na Uongozi wa Kata na Kijiji pamoja na kushiriki mazishi ya Marehemu kwa ajili ya kutoa Elimu ya uzazi salama.
Timu ya Watalamu wa Afya imefika katika Kata ya Mkomba Halmashauri ya Wilaya ya Momba, Kata ya Itaka Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi na Halmashauri ya Wilaya ya Songwe.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Dkt. Hamad Nyembea amesema wanafanya hivi kutekeleza maagizo ya Mkuu wa Mkoa, Omary Mgumba aliyotoa wakati wa kikao kazi cha kujadili vifo vya uzazi kwa robo ambacho Mkoa unafanya kila robo.
Mratibu wa Afya ya Uzazi Mkoa wa Songwe, Eva Mwakyusa amesema ufuatiliaji huu wa kifo cha mzazi unaanzia ngazi ya Kituo cha Afya ambapo kifo cha Marehemu kimetokea hadi kwenye jamii anapoishi ili kujua tatizo limetokea wapi na kuhakikisha halijitokezi tena.
Ikumbukwe kwa Mkoa wa Songwe kutoka Januari hadi Juni 2021 kumetokea vifo 12 vya uzazi ambavyo vilikuwa vinauwezo wa kuzuirika kama Mama mjamzito angefuata ushauri alioapewa na watalamu wa Afya, Gari la kubeba wagonjwa lingekuwepo kwa wakati na watalamu wa Afya kuchukua hatua za makusudi na kwa haraka kwa mujibu wa taratibu za taaluma yao
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.