Katibu Tawala Msaidizi Mpingo na Uratibu Ndg. John Mwaijulu amekuwa mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Dk. Francis Michael, katika hafla ya uzinduzi wa kampeni ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa polio iliyofanyika katika eneo la Mlowo, Wilaya ya Mbozi.
Katika hotuba yake, Ndg. John Mwaijulu alitangaza kwamba zoezi hilo la chanjo litafanyika kwa siku nne, kuanzia tarehe 21 hadi 24 Septemba 2023, na kuwataka wananchi wa Mkoa wa Songwe kuhakikisha watoto wao walio chini ya umri wa miaka 8 wanapata chanjo dhidi ya ugonjwa hatari wa polio.
Alisema, "Chanjo hii ni salama kabisa na itatekelezwa nyumba kwa nyumba, mashuleni, na katika nyumba za ibada. Natoa rai kwa wananchi wote kuepuka kuamini taarifa zozote za uzushi kuhusu chanjo hii."
Mwakilishi kutoka TAMISEMI, Ally Kananika, alitoa wito kwa wananchi kushiriki kikamilifu katika kampeni hii ya chanjo. Alisisitiza kuwa Wizara ya Afya na TAMISEMI zimejitolea kuhakikisha jamii inalindwa dhidi ya magonjwa yanayoweza kuzuilika kwa chanjo, na hivyo aliwasihi wazazi na walezi kuhakikisha watoto wao wanapata chanjo hiyo muhimu.
, Afisa Programu kutoka Wizara ya Afya, Penifored Joel, alisisitiza umuhimu wa wananchi kushiriki katika zoezi la chanjo na kuendelea kufuatilia chanjo kwa watoto wao hata baada ya kipindi cha kampeni kukamilika. Alieleza kuwa chanjo ni kinga ya kudumu dhidi ya ugonjwa wa polio na magonjwa mengine, na hivyo ni jukumu la kila mzazi na mlezi kuhakikisha watoto wao wanapata kinga hiyo.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.