VITUO VYA RASILIMALI KILIMO KUIMARISHWA KWA TEKNOLIJIA.
Na. Nicholas Ndabila
SONGWE: Serikali ya awamu ya sita imeongeza nguvu katika kuimarisha vituo vya Rasilimali Kilimo vilivyopo kwa zana za kisasa na teknolijia ili kupeleka teknolijia kwa wakulima wajifunze vizuri.
Hayo amesema Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Songwe, Bwn. Vanscar Kulanga katika hafla ya kukabidhi pawatila kwa Halmashauri ya Momba maalumu kwa ajili ya kituo cha Rasilimali Kilimo cha Kamsamba pamoja na kukabidhi dawa kwa ajili ya zao la Korosho ambalo linalimwa kwa Halmashauri ya Momba na Songwe, hafla imefanyika katika ofisi za Mkoa, Agosti 19.
Kulanga, amesema Serikali imejipanga ifikapo 2030 Kilimo kiweze kuchangia asilimia 10 ya pato la Taifa na kufika lengo ni kuimarisha vituo vya Rasilimali Kilimo vya Kata ili mkulima aweze kujifunza kwa vitendo.
"Tunataka kuona pawatila hii inakwenda kutumika kwa malengo yaliyokusudiwa, wakulima wa Kamsamba wakanufaike kwani inatakiwa iwe kwenye Kituo cha Rasilimali Kilimo cha Kamsamba" Vanscar Kulanga.
Ndg. Vanscar Kulanga amesema Serikali inataka kuona yanayofanyika katika maonesho ya Nanenane yafanyike kupitia vituo vya Rasilimali Kilimo vilivyopo kwenye kata ili mkulima aweze kujifunza vipando mbalimbali vya mazao mbalimbali pamoja na ufugaji wa kisasa.
"Kwa sasa Mkoa una vituo 3 vya Rasilimali Kilimo cha Kanga kilichopo Wilaya ya Songwe, Iganba cha Mbozi na Kamsamba cha Momba na Wizara ya Kilimo imeonyesha nia ya kutujengea vituo 12 kama hivyo kwenye kila Tarafa lengo ni teknolijia ya Kilimo iwafikie wakulima wengi zaidi" Ndg. Vanscar Kulanga.
Pia, RUWASA watapeleka maji kwenye vituo vyote Ili muda wote kuwe na shughuli za Kilimo na mifugo zinazoendelea, amesema, Vanscar Kulanga.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Momba, Dkt. Amani Kilemile amesema pawatila waliyopata itakwenda kupeleka teknolijia kwa wakulima na wafugaji wa Kata ya Kamsamba.
Wakati huo huo,Ndg. Vanscar Kulanga amekabidhi dawa lita 324 kwa ajili ya zao la Korosho kwa wakulima wa Halmashauri ya Wilaya ya Songwe na Momba.
Mkoa wa Songwe una hekta zaidi ya 200,000 zinazofaa kwa kilimo cha Korosho na hadi sasa ni hekta zipatazo 2,475 ambazo zimeisha limwa Korosho kwa Wilaya ya Songwe na Momba.
MWISHO.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.