WADAU WATAKA RASILIMALI ZIGAWIE VIZURI KUPATA MATOKEO MAZURI YA WATOTO.
SONGWE: Wadau wa maendeleo wametoa wito kwa Taasisi mbalimbali na Serikali kugawa Rasilimali vizuri kwa watoto ili matokeo chanya yapatikane.
Witu huo umetolewa kwenye Jukwaa la juu la kujadili changamoto, fursa na sera lililofanyika kwa mara ya kwanza Tanzania katika Mkoa wa Songwe 8 Septemba 2022.
Mwakilishi wa UNICEF Tanzania, Shalini Bahumuna amesema wadau tumekusanyika hapa ili kujifunza jinsi tunavyotekeleza sera kwa kugawanya vizuri Rasilimali na kupata matokeo bora kwa watoto, Wanawake na familia zao.
Shalini Bahumuna amesema ni swala la kutumia Takwimu zetu vizuri na kufanya maamuzi sahihi kwa kutumia Rasilimali chache zilizopo na kuboresha matokeo katika sekta za kijamii kama Elimu na Aya.
"UNICEF hatuwezi kufanya pekeyetu ni lazima sote tushirikiane ndio maana leo zipo Wizara za kisekta kama OR TAMISEMI, Elimu, Fedha na Mipango pamoja na wadau wengine wa maendeleo wa ndani na nje ya Nchi" Shalini Bahumuna Mwakilishi wa UNICEF Tanzania.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Songwe, Ndg. Elynico Mkola amesema watoto wenyewe ndio waanzilishi wa harakati za kudai elimu na haki zao miaka ya 1970 Soweto Nchini Afrika Kusini sisi kama wazazi na walezi tuna deni kubwa la kuwasaidia sasa.
"Chama kitasaidia kuwaeleza wananchi kuhusu mambo yote ambayo wamekubaliana kwenye kikao cha wadau" Ndg. Elynico Mkola.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Waziri Kindamba amesema pamoja Songwe inazalisha sana chakula lakini bado kuna tatizo la udumavu kwa watoto wa umri chini ya miaka 5 kwa 43% ukilinganisha na wastani wa kitaifa wa 32%.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Juma Homera amezishauri Halmashauri kutenga Bajeti kwa ajili ya kusaidiana na wadau katika kuboresha elimu kwa kutoa mafunzo kwa waalimu na kutatua upungufu wa waalimu.
Mhe. Juma Homera amezitaka Halmashauri kutotegemea kila kitu kifanywe na Serikali kuu, kwani Serikali kuu imejenga miundombinu mingi ya Elimu pamoja na kulipa mishahara ya watumishi.
Halmashauri lazima ziwe na mkakati wa kuweka Bajeti katika sekta ya Elimu kwa ajili ya kupata waalimu wa muda mfupi ambao wapo mtaani na wamehitimu vizuri, hii itamsaidia sana Mhe. Samia Suluh Hassan Rais wa Tanzania katika kutatua changamoto kwa wananchi wake.
MWISHO.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.