WAKULIMA WATAKIWA KUWATUMIA VIZURI MAAFISA UGANI.
SONGWE: Serikali metoa wito kwa wakulima nchini kuwatumia vizuri Maafisa ugani ambao wako kila kijiji na Kata ili wakulima waweze kulima kwa tija na kwa Biashara.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mhe. Queen Sendiga wakati akimuwakilisha Waziri wa Kilimo kwenye kilele cha siku ya Mbolea Duniani ambayo kitaifa imefanyika Mkoa wa Songwe katika viwanja vya Kimondo wilayani Mbozi.
"Serikali ya Mhe. Samia Suluh Hassan imeweka maafisa ugani katika ngazi za kata na vijiji na maafisa ugani wamepewa usafiri na vifaa vya kitaalamu vya kupimia udongo nitoe rai kwa wakulima kuwatumia wataalamu hawa ili kuinua Kilimo chetu" Mwakilishi wa Waziri wa Kilimo, Mhe. Queen Sendiga Mkuu wa wa Mkoa wa Rukwa.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mhe. Queen Sendiga ametoa wito kwa wakulima kuendelea kujisajili kielektroniki kwa ajili ya kupata Mbolea ya Ruzuku kwa kuwa zoezi ili halina mwisho kwa sasa.
Aidha, Mhe. Queen Sendiga ametoa rai kwa viwanda vya Mbolea ambavyo bado havijakamilika kuongeza kasi ya kukamilisha ili Mbolea iingie sokoni kwani mahitaji ya Mbolea ni makubwa ukilinganisha na viwanda vilivyopo.
Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe. Samia Suluh Hassan iko tayali kumsaidia mfanyabiashara yeyote mwenye kiwanda cha mbolea kuhakikisha ana kamilisha ujenzi wa kiwanda, kwani lengo la Serikali ni kuwasaidia wananchi kupata Mbolea kwa urahii na wepesi zaidi, amesema Mwakilishi wa Waziri wa Kilimo, Mhe. Queen Sendiga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa.
Kwaupande wake Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe. Waziri Kindamba amesema usalama wa chakula unatakiwa kupewa kipaumbele na ndio sababu Mhe. Samia Suluh Hassan ameamua kutoa fedha kwa ajili ya Mbolea ya ruzuku ili Kila mkulima apate Mbolea ya bei nafuu na kupata chakula kwa ajili ya familia yake na Taifa.
MWISHO.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.