WANANCHI WA SONGWE KUPATA CHANJO YA UVIKO-19 YA AWAMU YA PILI.
SONGWE. Baada ya Jana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kuzindua chanjo ya UVIKO-19, Wananchi wa Mkoa wa Songwe wataanza kupata chanjo ya UVIKO-19 ya awamu ya pili kutokana na Mkoa wa Songwe haukupata madhara makubwa ya UVIKO-19 kama Mikoa ya Dodoma, Dar es Salaam, Mbeya, Kilimanjaro, Mwanza, Mara, Geita, Arusha na Kagera.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Dkt. Hamad Nyembea amesema chanjo ya UVIKO-19 kwa awamu ya 2 itatolewa kwenye Kila Halmashauri kwa vituo ambavyo vitafahamika mara baada ya chanjo kuwasili.
Aidha, Dkt. Nyembea amesema wataanza na makundi ya kipaombele kama Waalimu, Watumishi wa Afya, wenye umri kuanzia miaka 45 na kuendelea na Wenye magonjwa ya kudumu.
Wakati Mkoa unaendelea na maandalizi ya kupokea chanjo ya UVIKO-19 ambayo itatolewa bure wananchi wametakiwa kuendelea kuchukua tahadhari ya kujikinga na UVIKO-19 kwa kufuata ushauri wa watalamu wa Afya.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.