WANANCHI WAHAMISHIA SHULE KARIBU NA MAKAZI YAO.ILEJE:
Wananchi wa Kijiji cha Msia Kata ya Chitete wamejenga vyumba 9 na ofisi 4 ili kukamilisha lengo lao kuhamisha Shule ya Msingi Msia na kuiweka karibu na Makazi kutokana na Shule ya zamani kuwa mbali na makazi na kukatika kwa mawasiliano kipindi cha mvua kutokana na eneo ilo kujaa maji.Pamoja na nguvu za wananchi, Serikali kuu imeleta fedha milioni 37 kwa ajili ya ukamilishaji wa vyumba vya madarasa, Halmashauri ya Ileje imetoa Milioni 20 pamoja na nguvu za wadau mbalimbali.Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Omary Mgumba amewapongeza wananchi wa Msia kwa jitihada zao kujiletea maendeleo.Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Mhe. Anna Gidarya amesema wanafunzi wa Shule ya Msingi Msia wataanza kusoma kwenye shule mpya Septemba 2022 baada ya zoezi la Sensa na makazi kukamilika.MWISHO.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.